Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, akipeana mkono na Mkuu wa shule ya sekondari Doma , John Makarius kama ishara ya kukabidhi msaada wa viti 100 kwa shule hiyo , Mbunge huyo alitoa ahadi kuipatia viti hivyo alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne mwaka jana.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, akimkabidhimfuko mmoja kati ya 50 ya saruji , Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Doma, Wilayani humo, Mkoani Morogoro, Salum Malinza ,wakati ( kulia ) ni Diwani wa Kata ya Doma, Elimu Kisuguru , Mbunge huyo alitoa msaada wa saruji hiyo ili kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa ya mkondo wa shule ya Msingi Doma.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( aliyenyosha mkono) akisisitiza namna ya kuendeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa ya mkondo wa shule ya Msingi Doma, Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, (aliyeko mbele yake ) ni Diwani wa Kata ya Doma, Elimu Kisuguru, Mbunge huyo alifanya ziara katika Vijiji vya Maharaka na Doma ,vilivyopo Wilayani humo na kukabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi .
Nahodha wa timu ya soka ya Usipime ya Kijiji cha Doma , Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro,Salum Mkerewe ( kulia) akipokea msaada wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira miwili na seti moja ya jezi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, juzi alipowatembelea wananchi wa Kijiji hicho.
Nahodha wa timu ya soka ya Wasuni ya Kijiji cha Maharaka , Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro,Hamis Mkono ( kulia) akipokea msaada wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira miwili na seti moja ya jezi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, juzi alipowatembelea wananchi wa Kijiji hicho.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kati kati ) akifurahia jambo wakati akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Maharaka, Kata ya Doma , Wilayani humo ( kulia ) ni Diwani wa Kata ya Doma, Elimu Kisuguru, Mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwashukuru kwa kumchangua kuwa mbunge wao.
No comments:
Post a Comment