IMEELEZWA kuwa Vurugu zilizotokea jana Mkoani Morogoro na kumhusisha Msanii wa Nyimbo za Bongo Fleva Afande Sele pia zilimhusisha Msanii mwingine wa nyimbo hizo aliyejizolea Tuz lukuki katika Tuzo za 2011 za Kili Music Award 20% ambaye pia yupo katikia kundi la Watu Pori chini ya Afande Sele.
Blog hii bado inaendelea kusaka taarifa zaidi kuhusiana na vurugu hizo zilizopelekea Polisi kutawanya watu kwa Mabomu ya machozi na Risasi, katika jirani na Benki ya NMB tawi la Wami hadi Polisi kufyatua risasi angani kutuliza vurugu hizo.
Inadaiwa kuwa ugomvi huo ulianzaia mbali baina ya Kundi la Watu Pori na vijana wengine jambo ambalo lilipelekea Watu Pori kuwatafuta vijana hao kwa mapanga, marungu na fimbo, na walifika hapo Wami vifua wazi.
Habari pia zilizoifikia Blogu hii hivi punde ambazo ni za kipolisi zinadai kuwa taarifa ya Polisi inasema kuwa vijana hao wa kundi la Watu Pori wakiwapo wasanii hao wawili, Afande Sele na 20% wanakabiliwa na tuhuma za kutaka kufamnya uhalifu katika Benki ya NMB, jambo ambalo linadaiwa kuleta utata kwa wananchi ambao baadhi yao walikuwa mashuhuda wa tukio hilo.
Inadaiwa kuwa wasanii hao walijeruhiwa vibaya katika vurumai hiyo. Ambayo wadau wanasema si picha nzuri kwa Afande Sele ambaye hivi karibuni aliweka bayana nia yake ya Kutaka kugombea Ubunge katika uchaguzi Mkuu Ujao wa 2015.
Kwamujibu wa shuhuda wa tukio hilo anapasha kuwa awali vijana hao wanaodaiwa kuwa ni wapambe wa Afande Sele, walitinga wakiwa katika gari dogo na kuliegesha jirani na Benki hiyo kasha kuteremka wakiwa na mapanga mkononi jambo ambalo liliwastua askari Polisi waliokuwa lindoni katika benki hiyo.
Aidha baada ya muda mfupi huku Polisi hao wakila mingo walishanga kutokea vurugu kubwa katika moja ya vibanda hivyo, na kuwatia nguvuni vijana hao na Polisi kushikilia gari hilo kwa hatua zaidi.
Shuhuda huyo anasema vijana hao walipokuwa chini ya ulizni ili polisi wengine waje kuwachukua pamoja na gari walilokuja nalo walidai gari ni mali ya Afande Sele hivyo wamuite aje kulichukua.
Simu ikapigwa kwa Afande Sele na alipofika alitaka achukue gari lake na hao vijana waende nalo, lakini Polisi walesema gari hilo halitatoka ndipo vurumai nyingine ikaanza katika eneo hilo.
Shuhuda napasha zaidi kuwa walifika Polisi wa doria majira ya saa kumi na mbili jioni eneo la tukio kutokana na vurugu hizo zikafyatuliwa risasi huku mawe yakirushwa jambo lililopelekea kuharibika kwa magari kadhaa.
No comments:
Post a Comment