Wapendwa wasomaji na wapenzi wa Blogu ya FATHER KIDEVU naomba niwashirikishe maoni haya ya mdau mwenzetu ambayo aliyatoa katika moja ya machapisho yaliyopo humu. FK Blog ikaona ikibaki tu kama maoni si wote tunapenda kusoma nani katoa oni gani juu ya habari husika, ila pia tuwe tunatoa maoni/ushauri kwani kufanya hivyo kutaleta maendeleo baina yetu.
MAONI YA MDAU wetu aliyejitambulisha kwajina moja la HELLEN ni kama hivi....
Poleni sana wote mlioguswa na msiba wa Jane.
Ila napenda kutoa maoni yangu kidogo kuhusiana na kauli ya kusema kwamba "Amsalimie mumewe huko, na bila shaka kampokea kwa shangwe sana". Kauli kama hizi zimejengwa katika akili za wengi, kutokana na mafundisho ya viongozi wa dini za Kikristo duniani, zinazofundisha kwamba mtu akifa anakwenda mahali fulani. (Mbinguni).
Kwa sisi tunaoiamini Biblia, inasema hivi: Wafu hawajui neno lolote...... Mhubiri 9:5-10.
Mtu anapokufa anarudi mavumbini. (Mwanzo 3:19 ;Mhubiri 3:20 ; Mwanzo 47:30 ; Zaburi 88:10 ; Zaburi 15:17 ; Zaburi 146:4 ; Isaya 38:18 ; Yohana 11:11.) Kwa sababu wote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, ndio maana tunakufa Warumi 5:12.
Wanasubiri ufufuo utakaofanywa kupitia Mfalme Yesu kristo (Yohana 5:28,29)Maneno kama "Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana na libarikiwe" yamenukuliwa kutoka kwa Ayubu (Mhubiri1:21) Ayubu aliyatamka maneno hayo AKIDHANI kwamba ni Mungu aliyesababisha mateso yake.
Kumbe ni Shetani Ayubu 1:6-20. Hivyo hivyo leo, mengi machungu yanapotupata "tunamsingizia Mungu" kwamba ni mapenzi yake. Kwa mfano, mtu anakunywa pombe kupita kiasi, anaendesha gari, anagonga mti, anakufa.
Utasikia maneno kama:- "Kama aliandikiwa kufa kwa aksidenti lazima afe tu!", "Mungu amempenda zaidi", "Mungu amechukua kiumbe chake", "Mungu amechuma ua lake", n.k.Hembu tutafakari. Mungu amezuia ulevi, kwa hiyo kama asingekuwa mlevi kwa kutii aizo hilo, angeendesha kwa uzembe agonge mti?..... Na je, Mungu anajisikiaje anapotajwa kuwa ndiye msababishi wa kifo hicho?.... Kama ungekuwa wewe, ungejisikiaje?
Ndio maana katika sala ya Bwana ya kielelezo, tunasali Jina la Mungu litukuzwe litakaswe),(Mathayo6:9,10) maana limelundikiwa lawama nyiiingi isivyo haki.
No comments:
Post a Comment