Kwa niaba ya familia ya KAPINGA, Ningependa kutoa shukrani kwa wote walioshiriki kwa hali na mali kwenye msiba wa mdogo wangu Dennis Kapinga, aliyefariki saa 8.10 mchana wa Jumanne ya Machi 27 kwenye hospitali ya Mwananyamala.
Ni vigumu kumshukuru kila mmoja kwa kutaja jina, lakini basi angalau nichukue fursa hii kuwashukuru wote walioweza kufika na kuungana nasi na wale walioshindwa kufika, lakini walitufariji kupitia salamu zao. 40 ya marehemu itafanyika tarehe 2/6/2012.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu Dennis Kapinga.
Joseph Kapinga
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment