April 05, 2012

ratiba ya Msondo Pasaka hii

BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika kusherekea Siku kuu ya Pasaka ambapo wamesema kuwa wataanza leo kutoa burudani ndani ya Wipes Bar Mivinjeni Kurasini, siku ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosi watakuwa TCC Club Chang’ombe, Pasaka watakuwa Kata ya 14 Temeke na Jumatatu ya Pasaka watakuwa sambamba na FM Academia ‘Wazee wa ngwasuma’.

Akingongea , Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea ndani ya bendi yao.

Alisema kuwa hata hivyo tayari wamajipanga vizuri katika suala zima la kuwapa burudani mashabiki wao katika kusherekea sikukuu hii  ya Pasaka.

“Msondo ipo kamili katika kutoa burudan na ndiyo maana imeamua kutoa ratiba, hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye matamasha yetukwani bila wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa wanahitaji mashabiki wao kjitokeza kwa wingi ili waone nini wanachowapa katika siku hizo zote kwani sikukuu ya pasaka ni muhimu kusherekea na msondo ngoma bendi hiyo inayotamba
  na vibao vyake vipya vya Suluhu wa Shabani Dede na Nadhiri ya Mapenzi wa
Juma Katundu pia watapiga nyimbo zao zote zilizotamba kipindi cha nyuma alisema Super D

No comments:

Post a Comment