April 07, 2012

Okwi aibeba Simba Algeria

 Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi akiambaa ambaa na mpira wakati wa mchezo wa awali dhidi ya ES Setiff ya Algeria jijini Dar es Salaam. Okwi aliifungua Simba goli la kufutia machozi nchini Algeria na kuivusha Simba katika mzunguko mwingine.
 
Timu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam,leo imefanikiwa kusonga mbeke kwa hatua nyingine katika masindano ya Kombe la Shirikisho.Timu hiyo ambayo ilikuwa imejitupa dimbani jioni ya leo huko nchini Algeria kucheza na timu ya Es Satif ya nchini humo ambapo matokeo ya mchezo huo (Es Satif 3 - 1 Simba SC) ndio yameipa nafasi ya kusonga mbele timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam.

Timu Simba imeweza kusonga mbele baada ya kupata bao la ugenini lililotiwa kimiani na Mshambuliaji Machachari wa Simba,Emmanuel Okwi (dk 91) wakati hapo awali Simba iliifunga timu ya Es Satif bao 2 - 0 nnyumbani.

1 comment:

  1. Teuvo Kuvat- Teuvo Images Finland visited this blog. Come and visit my blog . You should also tell your friends to my blog Teuvo Vehkalahti Finland

    ReplyDelete