Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akiwa ameketi kwenye Kigoda akiombewa Dua ni Chifu wa Kabila la Wabende Chifu Victor Mfinula kabla ya kutunukiwa uchifu wa kabila hilo jana baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa Mpya wa Katavi.
Katibu Tawala wa Mkoa Mpya wa Katavi, Injinia Emmanuel Kalobelo, Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na viongozi wengine wakiwa kwenye moja ya Sala zilizoongozwa na viongozi wa Dini waliohudhuria hafla hiyo.
Wananchi wengi wa Katavi walijitokeza kumlaki Kiongozi wao Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe na Katibu Tawala Mkoa huo Injinia Emmanuel Kalobelo
Hapa ni Mpakani mwa Mikoa ya Rukwa na Katavi kwenye Mlima maarufu wa Lyamba Lyamfipa. Utawala wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya unaishia hapa, anashusha kibendera kuruhusu Utawala Mpaya wa Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe kupandisha bendera yake tayari kuipepeza kwenye Milima na Mabonde ya Utawala wake Mpya wa Mkoa Mpya wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wananchi wa Mkoa Mpya wa Katavi waliojitokeza kwa wingi kabla ya kuwatambulisha viongozi wao katika uwanja wa Mpira wa Kashaulili uliopo Wilayani Mpanda. Aliwaomba wananchi hao kuwapa viongozi wao wapya ushirikiano wa dhati ili kurahisisha utendaji kazi wao kwa maendeleoa ya Katavi na Ukanda mzima wa Ziwa Tanganyika.
Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akihutubia wananchi wake wa Mkoa Mpya wa Katavi mara baada ya kutambulishwa kwao na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Aliwaahidi ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha Katavi inasonga mbele.
Safari ya kuelekea makabidhiano ilianza ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambaye alianza kwa kumuombea dua Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Rutegwe mapema kabla ya kuanza safari kuelekea Wilayani Mpanda Mkoa Mpya wa Katavi ambapo ndipo yalipofanyika makabidhiano hayo. Mkoa wa Rukwa umegawa na kuundwa Mkoa Mpya wa Katavi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kusogeza huduma zake kwa wananchi. Kwa pamoja viongozi wote wa Mikoa ya Rukwa na Katavi wameishukuru sana Serikali ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuugawa Mkoa wa Rukwa kwa maslahi ya wananchi wake.
No comments:
Post a Comment