April 07, 2012

Lulu atajwa kifo cha Kanumba

Elizabeth Michael a.k.a Lulu
Ndugu wa Kanumba akihojiwa.
TAARIFA kutoka kwa ndugu wa Marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa akiishi nae Sinza jijini Dar es Salaam na wakati mauti yanamkuta Kanumba alikuwapo nyumbani hapo zinasema chanzo cha kifo chake ni ugomvi baina ya kanumba na Msanii mwingine wa kike ambaye ni rafiki yake.

Ndugu huyo amepasha kwa wanahabri kuwa Msanii huyo wa kike ambaye analikuwa na mahusinao na marehemu kuwa ni Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu.

Akisimulia kwa ufupi chanzo cha kifo hicho cha Ghafla cha Nguli wa Filamu za Kibongo “ Bongo Movie” anasema wakiwa hapo nyumbani alifika Lulu majira ya usiku.

Anasema aliwaacha wawili hao wakizungumza klakini baade alisikia kuwepo kwa malumbano na wakahamia chumbani ugomvi ukazidi kuendelea. 

Anasema kuwa mara alitoka Lulu na kumita yeye na kumwambia kuwa kanumba ameanguka na alipoingia chumbani humo alikuta kweli ameangua na ndipo alichukua uamuzi wa kumtafuta daktari wake aje kumtibu.

Anasema ndugu huyo kuwa wakati ameruidi ndani humo na Daktari Lulu alikuwa amesha toweka ndipo wakachukua mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya taifa Muhimbili ambako mwili wa marehemu ulihivaziwa hadi hivi sasa kuendelea na uchunguzi zaidi.

Aidha habari zaidi zinasema kuwa tayari mwana dada huyo maarufu katika ulimwengu wa Filamu za Bongo yupo mikononi mwa Polisi na alikuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Mkoa wa kipolisi cha Kinondoni pale Oystebay Polisi jijini Dar es Salaam.

Hivi karibuni katika kipindi cha Mikasi kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Channel 5 Lulu mbali na mahojiano mengine aliulizwa juu ya uhusiano wake na msanii huyo na kukataa kata kata kuwa hana mahusiano nae ya kimapenzi isipokuwa ni usanii pekee ndio unawaweka karibu.

Tutaendelea kuwaopasha zaidi juu ya mkasa huu. Lakini niwazi kama kweli Lulu alikuwepo nyumbani hapo na katika purukushani za kutofautiana na Kanumba ndio zimepelekea kifo chake basi atafunguliwa mashitaka na huenda ikawa ni mauaji pasi kukusudia inategemea na uchunguzi utakavyo fanyika. 

15 comments:

  1. RIP Kanumba roho inaniuma sana.

    ReplyDelete
  2. Mimi na swali mmoja je kama ni yalikuwa ni mahusiano ya kisanaa tu je ilikuaje hadi Lulu akaingia chumbani mwa Kanumba?

    ReplyDelete
  3. Ngoja tusubiri tuone itakuwaje?

    ReplyDelete
  4. sheria ichukue mkondo wake

    ReplyDelete
  5. KISWAHILI KIBOVU BWANA EDITOR, CHECK YOUR WORK

    ReplyDelete
  6. Katus wa mabiboApril 08, 2012

    Akionekana anayohatiya achukuliwe hatua kali

    ReplyDelete
  7. may be/yamkini inzi kafia kwenye kidonda.serikali itamua nini cha kufanya.

    ReplyDelete
  8. Lulu asilaumiwe jamani...owkay inawezekana amesababisha kifo bt 2simlaumu kwani Kanumba angekufa tu,yeye ni mwanadamu....wanasheria wanawake,angalieni swala hli kwa ukaribu jamani

    ReplyDelete
  9. RIP kanumba,ila tukumbuke kuwa kifo ni kifo ila sababu ya kifo ndio inayoleta utata,hatupasi kumuhukumu binti wa watu kwani sisi wote hatukuwepo kwenye tukio,hivyo anayejua ukweli ni lulu na muumba wake hivyo tuwe wavumilivu ktk kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  10. UKWELI WOTE UTAFAHAMIKA THOUGH KANUMBA ASHAFARIKI. HATUTAKIWI KULUMBANA KUHUSU KIFO CHAKE CHAMNO TUMUOMBEE ILI APOKELEWE KWA MUNGU. MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI AMINA

    ReplyDelete
  11. I would ask her if she n him got in fight first. If not, how did LULU react toward this incident??? Free fall is dangerous for the skull. Here is another question, Was the floor slippery???? Can one infer that Kanumba was pushed??

    ReplyDelete
  12. We were excited to receive him here in the USA. We always treat brother and sister visitors fairly with joy. We now shocked. May justice work this case out through.

    ReplyDelete
  13. Poleni wafiwa, kumbukeni mauti nayo pia yameumbwa na lazima yaishi, so tuache kutafuta mchawi kwenye hili mana alichopanga Mungu mwanaadamu Hawezi kukitengua. Mpeni pole dada lulu kwa mitihani mana yore tumeumbiwa sisi wanaadamu. Tujihadhari tusijekumkosa huyo dada kwa frustration na hukumu isiyothibitishwa

    ReplyDelete
  14. Waungwana wanasema kila jambo lina sababu, so tuache dada wa watu a pate fair justice.

    ReplyDelete
  15. pia tuangalie kwa kina maybe ilikua by accident,it was not her willing jamani. let's wait. but remember God is the true judge.

    ReplyDelete