April 13, 2012

Kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine, yafanyika Morogoro

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Mideye akishiriki katika ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12, 2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu, Mstaafu, Edward Lowassa katika Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati  Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki, Kigango cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12,2012.  Watatu Kushoto ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Mideye akimwombea marehemu Sokoine.
 Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Mhasham Telsphor Mkude  akibariki sanamu ya aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine  kwenye viwanja vya Kikagango cha Kanisa hilo katika kijiji cha Wami Sokoine , Morogoro baada ya kuongoza Ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo Aprili 12,2012.
 Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude akiteta na Namelok Sokoine, Binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum katika ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo iliyofanyika kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine,Morogoro Aprili 12,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor  Mkude  baada ya Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye kanisa katoliki, Kigango cha Wami Sokoine Aprili 12, 2012.  Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na watatu kulia ni Binti wa Marehemu Soine, Namelok Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum

No comments:

Post a Comment