April 09, 2012

CHEGE ACHENGUA AMSTERDAM

Mwanadada aliyekuwa amenogewa na makorombwezo ya Tmk alishindwa kabisa kujizuia na kujimwayamwaya na Chege kama unavyomuona. 
Chege chigunda akiendelea libeneke la makamuzi stejini,huku mashabiki wake wakiwa sambamba na nyimbo au mistari
Msanii wa kike toka Uganda kwa jina anaitwa Jackie Chambiru aliripua ukumbi kwa mayowe kwenye show yake iliyopendeza kabisa
Ndugu yangu Kamanda Kessy kushoto alikuwa na rafiki yake ambaye anaupenda sana mziki wa Bongo Fleva alikuwa ni kujimwayamwaya tu ndani ya show ya Chege.
Na huyu ni msanii mwengine wa Uganda ambaye alipendezesha sana show na kushangiliwa na umati uliofika kwenye show hiyo hapo jana.
Wakaanga mambo ya muziki wakibadilishana mawazo jinsi gani ya kuufurahisha ukumbi
Bishoo wangu wa Holland kijana Yusuf nae pia alikuwepo mjengoni kumshuhudia kijana Chege
Msanii mwingine toka Ug ambaye alitumbuiza kwa staili kemkem zilizowachengua washabiki.
Haji Mrisho msanii kutoka Uganda alikonga nyoyo za mashabiki ukumbini pale kwa nyimbo zake alizokuwa akiimba,kwa kweli show nyingi ziliburudisha watu ukumbini pale.
Picha na  MGANGAONE BLOG

No comments:

Post a Comment