April 15, 2012

Askofu mpya wa Anglikana Zanzibar asimikwa

 Askofu Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.ValentinoMokiwa,(kulia)akimtambulisha kwa waumini Askofu wa Kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh,baada ya kumalizika ibada maalum ya kumuweka Wakfu,katika Kanisa Kuu la Mkunazinileo.
 Askofu Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa,(kushoto) akimuweka Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la   Mkunazini, Mjini Unguja jana.   

 Askofu wa  Mkuu wa  Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa,(aliyesimama) akimuweka Wakfu Padre Michael Henry
Hafidh,(aliyelala) kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la  Mkunazini,  Mjini Unguja

Askofu Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa,(mbele) akiongoza maaskofu katika sherehe za kumuweka Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la  Mkunazini Mjini Zanzibar leo.


 Baadhi ya waumini wa Dini ya kristo Kanisa la Mkunazini Zanzibar,wakiwa katika sherehe ya kuwekwa wakfu Padre Michael Henry Hafidh,kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar,sherehe hizo zilifanyika jana katika Kanisa Kuu la Mkunazini Mjini Unguja.

Askofu Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa,(mbele) akiongoza maaskofu katika sherehe za kumuweka Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la  Mkunazini Mjini Zanzibar leo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake alipokuwa mgeni rasmi katika kafla ya ibada ya   kuwekwa Wakfu Padre Michael Henry Hafidh, kuwa Askofu wa Dayosisi  ya Zanzibar jana,katika hafla iliyofanyika Kanisa Kuu la Mkunazini Mjini Unguja.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipeana mkono na Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh,baada ya kuwekwa Wakfu wa Dayosisi hiyo jana,katika hafla iliyofanyika Kanisa  Kuu la Mkunazini Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa nne kushoto) Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa,Askofu Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya ibada ya kumuweka kuwa Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,(wa tatu kushoto) kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar katika  Kanisa Kuu la Mkunazini Mjini Zanzibar jana,(wa pili kushoto) Mke wa Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar Merry Michael.

No comments:

Post a Comment