March 24, 2012

Tamasha la michezo la wanahabari leo katika picha

Bonanza la Waamdishi wa habari (Media Day)linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari nchini (TASWA) linaendelea kwenye ufukwe wa Msasani Club Beach jijini Dar es salaam huku waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini wakiendelea na michezo mbalimbali, na kupata burudani za muziki. Wanahabari wanaonekana wenye furaha kwani bonanza hili linakutanisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali na hii ni siku pekee ambayo angalau wanahabari wanaweza kukutana na kubadilishana mawazo huku wakipata burudani. Bendi ya FM Academia ndiyo iliyopewa dhamana ya kuwaburudisha wanahabari huku mgeni rasmi akiwa mzee Samwel Sitta waziri wa Africa Mashariki na mbunge wa Urambo mkoani Tabora. Katika pozi ni Vimwana vya FM Academia vinavyotarajiwa kumwaga burudani kwa waandishi wa habari.

FULLSHANGWE iko katika eneo la tukio na inakumuvuzishia matukio moja kwa moja kutoka Msasani Beach Club kama unavyoniona mkurugenzi nikiwa kazini huku rafiki yangu Ras Joachim Kanyopa akiniangalia.
Mwandishi wa habari kutoka gaqzeti la Hoja Iche Mang'enya mzee wa Zengwe akimshushia kombora la ngumi Mpiga picha wa gazeti la The Express Said Khamis katika mchezo wa masumbwi uliokuwa siyo rasmi.
Mwalimu wa Masumbwi Super D. Mhamila akitoa maelezo kwa wachezji wa mpambano huo kulia ni  Said Khamis na Iche Mang'enya kabla ya mpambano wao.
Mdau Edo Kumwembe kulia Iche Mang'enya wakifurahia juambo.
Timu za Times na Busness Time zikichuana vikali katika mpira wa miguu.
Mdau Douglas Sagawala katikati akiwa na wadau Emmanuel Zinga kushoto na Freddy Chelelo.
Wadau kutoka gazeti jipya la Fahamu nao wamejivinjari katika bonaza hilo kama unavyowaona wakipozi kwa picha.
Hapa nikiwa na Mdau DJ Q wapili kutoka kushoto na washkaji wengine kutoka vyombo mbalimbali.
Wadau kutoka Mwananchi katikati ni Kalunde Vick kushoto na Ruth wakipozi kwa picha.
Michezo imepamba moto kama unavyoona katika picha.
Picha zote na Full Shangwe Blog. 

No comments:

Post a Comment