Mwimbaji wa muziki wa injili Solomon Mukubwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za Msama Promotion zilizoko Kinondoni Biafra wakati alipozungumzia uzinduzi wa albam yake mpya siku ya Tamasha la Pasana Aprili 8, 2012 inayokwenda kwa jina la Kwa Utukufu wa Mungu yenye nyimbo nane. Solomon Mukubwa amesema amejipanga kwa nguvu za mungu aliyempa kipaji cha uimbaji na anatarajia kumsifu mungu kwa nyimbo zake na kuwaalika mashabiki wa nyimbo za injili kwa kusema aprili 8 ni siku ambayo watu wanatakiwa kutua mizigo yao na kumpokea mungu. Mukubwa ametaja nyimbo zilizoko katika albam hiyo kuwa ni Kwa utukufu wa mungu wenyewe, Uaikate tamaa, Miungu wangu Nitetee, Moyo wangu tukuza bwana, Niko wa Yesu, Mke si nguo, Yesu jua zuri na Chunga ahadi yako.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdfjA4xL-MA-na1TVRU0DuaXioqbUeE0K_SEaQJD5T-J5SCokiipL5GrrsIj2QU-UYYVk622qu4rrp7UzZiXSAt24REiRNqbFx4P4MoAInR8tyfAkyKBCBM413iCKGxjZ8owOppKYkEwlY/s280/2.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhc7HfHu0sY1Q9NezNXxfImDK0gzLE7HuSGPRfygOSSGNEMhlkkQP_ET_SKSvlFybJs1V3dY_VGI5lxuWvpz7Hf0bFDcrO7USUduaLmV0OmYgfCvpe1Sm1BkJcVfAL0DJ9zk7k447o6dE65/s280/3.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyF7CC_8hUNo_9ARa4SjntQ9iEYV0HkWMfAC02dQppXVVb1jdbeRn1vnqbfpcZC-dauZx0CVl9lnlBbbUEqb1hpC-y85CvpkGDe26F0_Cc6ua_t8E6MFhklYBI5a_VnOlgJrgtLQRDy7_A/s280/1.jpg)
No comments:
Post a Comment