Rais Jakaya Kikwete leo amewasili Mkoani Iringa na kwenda moja kwa moja katika kijiji cha Itunundu kilichopo Kata ya Pawaga Wilayani Iringa umbali wa kilometa 75 kutoka Iringa mjini na kufungua mradi wa maji uliodhaminiwa na Kanisa la Aglikana Dayosisi Ruaha. Mradi huo wa maji safi umegharimu zaidi ya Sh Bilioni 2.15. Pichani ni Rais Kikwete akifungua koki kuzindua rasmi mradi huo wa maji.
Dk. Kikwete pia anataraji kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maadhimisho ya wiki yamaji Kitaifa Mkoani Iringa Machi 22,2012.
Rais Jakaya Kiwete akimtwisha Ndoo maji Bi. Agnes Mhavi mkazi wa kijiji cha Itunundu, mara baada ya Rais kuzindua mradi huo wa maji jioni ya leo Machi 21,2012.
Rais Jakaya Kiwete akimmsikiliza Askofu wa Dayosisi ya Ruaha ya Kanisa la Aglikana, Joseph Mgomi akimpa maelezo ya mradi huo.
Wananchi wakiwa katika uwanja wa Itunundu wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kuzindua mradi wa maji.
Moran wa Kimasai wakiimba nyimbo zao wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wa Mradi wa Maji kijijini hapo.
Rais Jakaya Kiwete akisalimia wananchi mbalimbali wa Kijiji cha Itunundu na vitongoji vyake waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo wa maji. Aidha tangu kijiji hicho kianzishwe miaka dahali iliyopita hakijawahi kutembelewa na kiongozi mkubwa wa Kiserikali.
Sehemu ya waanahabari waliofika Itunundu kuripoti tukio hilo la uzinduzi wa mraji wa maji.
No comments:
Post a Comment