Abdulham Gulam akipambana na Kagere Medie wa Rwanda kwenye mchezo wa Robo Fainali ya pili kwa siku ya leo ikiwa ni michuano ya kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 inayofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Tanzania. mpaka sasa mpira umekwisha ambapo Rwanda imeongeza goli la pili katika dakika ya 86 na kufanya matokeo ya mchezo huo kwa magoli 2-1. Matokeo haya yanaifanya Zanzibar Heroers kufungasha virago na Watanzania kubakiwa na timu moja tu ya Kilimanjaro Stars ambayo itashuka dimbani kesha kuikabili Malawi.
Ramadhan Agab wa timu ya Sudan akichuana na Kaze Gilbert wa timu ya Burundi katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Timu ya Sudan imeichapa Burundi magoli 2-0 na kuifurumusha nje ya mashindano.
Amin Suliman(kulia na )Muawia Koko wa Sudan wakimdhibiti Nigizimana Karimu wa Burundi katika mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wazir Salum wa Zanzibar Heroers akijaribu kumzuia Ntamuhanga Tumaini wa timu ya Rwanda Amavubi katikamchezo wa robo fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
No comments:
Post a Comment