KATIKA GAZETI TANDO HILI UTAWEZA KUJIPATIA HABARI MOTO MOTO KATIKA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA NDANI NA NJE YA TANZANIA HASA YALE YANAYOGUSA MAISHA YA KILA SIKU YA MTANZANIA.LUGHA KUU INAYOTUMIKA HUMU NI KISWAHILI.
July 24, 2011
Waziri Mkuu azindua kisima cha maji msalato
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia wakati Padri Timothy wa Shirika la Missionaries of Precious Blood alipomtwika ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Msalato kitongoji cha Nyerere mkoani Dodoma baada ya kuzindua kisima na matangi ya maji yaliyojenhwa kwa msaada na Shirika hilo likishirikiana na wanafunzi kutoka Canada Julai 23, 2011Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Padri Timothy wa Shirika la Missionaries of Precious Blood kukagua kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada na Shirika hilo kwenye kitongoji cha Nyerere, Msalato, Dodoma Julai 23, 2011. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. James Msekela na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa Aggrey Mwanri. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua kisima cha maji katika kitongoji cha Nyerere, Msalato, Dodoma Julai 23,2011. Kulia kwake ni Padri Timothy wa Shirika la Missionaries of Precious Blood ambalo limejengwa kwa msaada kisima hichoWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na wanafunzi kutoka Canada ambao walishiriki katika kuchangisha fedha na kujenga kisima katika kitongoji cha Nyerere, Msalato, Dodoma. Alikuwa katika mkutano wa uzinduzi wa kisima hicho Julai 23,2011.
No comments:
Post a Comment