July 25, 2011

Timu ya wabunge ya POOL wakikabidhiwa zawadi

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akimpongeza mshindi wa jumla wa mashindano ya mchezo wa POOL George Simbachawene Mbunge wa Kibakwe (Kulia)  mara baada ya kuibuka mshindi wakati wa mashindano  ya timu ya bunge na combine ya TBL na TAPA yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma. Hafla hiyo fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi ilifanyika leo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akimkabidhi Kapteni wa timu ya  Bunge  Idd Azan ambaye ni Mbunge wa Kinondoni  (kulia) zawadi ya timu ya Bunge ya Pool ya kukubali kushiriki kwenye mashindano ya mchezo huo yaliyoandaliwa  na Chama Cha POOL Tanzania  (TAPA) yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma. Hafla hiyo fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi ilifanyika leo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Viongozi wa Serikali, wachezaji wa timu ya Pool ya Bunge na viongozi wa Chama Cha POOL Tanzania  (TAPA) wakiwa katika picha ya pamoja nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kukabidhiwa kwa zawadi za washindi wa mashinndano hayo yaliyoandaliwa  na TAPA yaliyofanyika jumamosi iliyopita mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment