August 16, 2008

HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA

Hayawi hayawi yaliyokuwa yakisemwa juu ya Bw Robert Shija Mipawa na Bi. Blandina Leticia Buluda sasa yamekuwa baada ya wawili hao kukata mzizi wa mti wa ukapera uliokuwa umestawi kwa muda mrefu na kufanya wenyechuki na vidhabidhabina kusema mengi juu yao. Wakiwa na nyuso za furaha Robert na Blandina leo saa 10:00 asubuhi walifunga pingu za maisha katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam. Maharusi Robert na Blandina wakiwa na mtoto wao McNtosh. Bwana harusi ni mfakazi wa Infocom Technology na bi harusi ni mfankazi wa The Guardian Limited makampuni haya yote yapo chini ya IPP Media.
SIKU YA SEND OFF YA BLANDINA BULUDA MSASANI BEACH CLUB DAR ES SALAAM
Tuko pamoja....!!!!!

Bi harusi alipokuwa akimkokota Bwana harusi mtarajiwa katika msosi.

10 comments:

  1. yaani mmeishi katika uzinzi miaka yote hadi mtoto ameshakuwa mkubwa ndio mnajidai kuoana? hiyo sio safi ikishampenda ni kuchukuwa kwa jumla tu sio kuishi muda mrefu kama mke na mume wakati hamojaoana na baada ya mtoto kuwa mkubwa ndio eti mnaoana si mngeendelea tu kuvunja amri ya sita!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Hii kali mbona mwanaume ndio kabeba maua kweli bongo tambarare mambo ya bouguet sio ya kwetu sasa kama tumeamua kuiga basi tufanye kieleweke sasa mwanaume anabeba maua kama mwanamke jamani kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  3. Wewe anony wa kwanza august 16 2008 unaonyesha ni jinsi gani huendi kwenye shughuli hizi za kijamii. Hapo bi harusi alipewa maua na MC akamwambia atakaepewa hilo ua basi ndieBwana harusi mtarajiwa na Bi harusi akafanya alivyoambiwa. Ushansomaaa????

    ReplyDelete
  4. MKUBWA TUMEONA UJIKO WAKO KWENYE BLOG YA HAKINGOWI KWAMBA UNAPIGA PICHA ZA UHAKIKA TUNAOMBA NUMBER ZAKO ZA SIMU TUKUTAFUTE
    ASANTE

    ReplyDelete
  5. Mswahili utamjua tu! Hakosi ujinga wa kukoment wakati yake yamemshinda! Maharusi wamependeza jama na hapa bottom line ni wamefunga ndoa hayo mengine hayawahusu!!!! Maharusi tunawatakia maisha mema na Mungu awabariki na kuwasimamia katika ndoa yenu.

    ReplyDelete
  6. Wamependeza sana sana.
    Jamani na Theresia Buluda yuko wapi??miaka mingi...na bi harusi kadumu Ipp the media toka miaka hiyo

    ReplyDelete
  7. hamna sababu ya mwanamme kutembea na maua, hata kama alipewa ya utambulisho angempa bestman ayaache mezani sio kuzunguka ukumbi mzima na maua
    bongo bwana!

    ReplyDelete
  8. huwezi kujua ameamua k utembea na maua labda anafuga nyuki jamani kila mtu na taaluma yake na flavor yake

    ReplyDelete
  9. jamani huyu Robert Shija sie yule wa dodoma ambae alishawahi kuoa tena kanisani miaka kama kumi na tano iliyopita

    ReplyDelete
  10. My sis Blandina waache waste me tu!

    ReplyDelete