Nafasi Ya Matangazo

July 12, 2015

MWANAMAMA aliyepata kuwa Mwenyekiti mwenza wa Bunge maalum la Katiba na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rasi Muungano, Samia Hassan Suluhu  ndie mgombea mwenza wa Dk John Pombe Magufuli katika mbio za kuwania Urais katika uchaguzi ujao. 

Wawili hao watachuana na wagombea kutoka Kambi ya upinzani ambao huenda mwaka huu wakasimamisha mgombea mmoja. 

Samia Hassan Suluhu alizaliwa  Januari 27, 1960 na ni Mbunge wa Jimbo la Makunduchi Zanzibar .
Pia Aliwahi kuwa Waziri katika wizara za Utalii, Biashara na Uwekezaji, Waziri wa Kazi Jinsia na Watoto  katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Mwaka  1966-1968, alisoma shule ya msingi Chwaka mjini Unguja na mwaka 191970-1971 alisoma shule ya Msingi Ziwani, Pemba na kuhamia Mahonda Shule ya Msingi mjini Unguja mwaka 1972.

Mwaka 1973-1975 alisoma Sekondari ya Ngambo mjini Unguja, na mwaka 1976 Lumumba nayo ya Unguja.

Mwaka 1989 alisoma National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan, Institute of Management for Leaders, Hyderabad  India 1991 na Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA         1983.

Mwaka 1983-1986 alisoma Taasisi ya Uongozi Mzumbe (IDM) sku hizi Chuo Kikuu Mzumbe.

Na kasha akaenda Chuo Kikuu cha Manchester, London mwaka 1992 - 1994

Baade mwaka 204-2005 alikua Chuo Kikuu Huria cha Southern New Hampshire, USA

Posted by MROKI On Sunday, July 12, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo