Nafasi Ya Matangazo

November 07, 2014

.. 
                                       DC Mufindi Evarita Kalalu 
 Na matukiodaima.co.tz
SERIKALI  wilayani Mufindi  mkoani  Iringa imeipongeza  shule binafsi ya  Southern Highlands Mafinga kwa   kuongoza kiwilaya na  kuwa shule ya 8 kimkoa katika matokeo ya mtihani wa Taifa  wa darasa la saba mwaka  2014 .

Akitoa pongezi hizo hizo  mkuu  wa wilaya ya  Mufindi Evarista Kalalu  alisema  kuwa shule  hiyo  imeendelea kuipa heshima  kubwa  wilaya ya Mufindi 

 " Kilichofanywa na shule  hii ya Southern Highalnds  ni heshima  kubwa kwa shule  yenyewe  ila  ni  heshima ya  wilaya  nzima  mkoa na hata taifa  katika kuonyesha  uwezo mzuri  wa  walimu na  watumishi  wote wa  shule hiyo ......amini huu ni mfano  mzuri  kwa  shule  nyingine kuiga kwani baadhi ya  shule  binafsi  badala ya  kupanda katika ufaulu  zimeendelea  kushuka huku shule  hii  yenyewe  ikizidi  kufanya  vema...kweli nawapongeza  sana  walimu na uongozi mzima wa Southern Highalnds kwa  matokeo mazuri"
 
Hata  hivyo  mkuu  huyo  wa  wilaya  aliwataka  walimu wa  shule  zote  wilayani Mufindi kuendelea  na moyo wa  kujituma katika ufundishaji  ili  kuzidi  kuongeza kasi ya ufaulu katika  shule  zote za msingi na sekondari ndani ya  wilaya  hiyo.

Alisema  kuwa sifa  na ubora  wa elimu   inayoendelea  kutolewa katika shule   hiyo ya Southren  Highalnds Mafinga  inatokana na umakini na mkurugenzi  wake Bi Mary Mungai ambae amepata  kuwa afisa  elimu katika  wilaya  hiyo na wilaya nyingine nchini .

"Anachokifanya mkurugenzi  wa  shule  hii ni  kuendelea  kuonyesha  umakini  wake katika taaluma na ingekuwa si vema kama  shule  hiyo  ingeendelea  kufanya  vibaya  ila katika  kuhakikisha  kuwa  wazazi  wanaopeleka  watoto  wao hapo  hawajapotea ni baada ya kuendeleza ufaulu mzuri zaidi"

Kalalu  aliwataka   wazazi  wa  wanafunzi  waliofaulu katika  shule  hiyo na  wengine  wote  kuhakikisha  wanajiandaa kuwapeleka  watoto  wao  sekondari muda  utakapofika  badala ya  kuwaacha  watoto hao kukaa majumbani ama  kwenda  mijini kufanya kazi za ndani na uzululaji.
Posted by MROKI On Friday, November 07, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo