Nafasi Ya Matangazo

August 17, 2013

BAO pekee la kiungo Salum Abdul Telela jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC na kutwaa Ngao ya Jamii.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Oden Mbaga, aliyesaidiwa na Hamisi Chang’walu na Omar Kambangwa wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Yanga ilipata bao hilo mapema tu dakika ya pili, mfungaji kiungo Salum Abdula Telela aliyeunganisha pasi ya Didier Kavumbangu.

Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea kucheza vizuri na kukosa mabao zaidi, huku sifa zaidi akistahili kipa chipukizi Aishi Manula.

Dakika ya 67 Telela alikarbia kufunga tena baada ya kuunganishia nje krosi nzuri ya Haruna Niyonzima.

Dakika ya 81 Niyonzima alikaribia kufunga mwenyewe kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake liligonga mwamba wa juu na kudondokea chini kabla ya beki Aggrey Morris kuondosha katika hatari.

Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Deo Munishi ‘Dida’ dk15, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Mbuyu Twite dk15, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Salum Telela, Jerry Tegete/Hussein Javu68, Didier Kavumbangu na Haruna Niyonzima.

Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni/Joackins Atudo dk46, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Gaudence Mwaikimba dk74, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk62 na Khamis Mcha. SOURCE: BIN ZUBERI BLOG.
Posted by MROKI On Saturday, August 17, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo