Nafasi Ya Matangazo

August 13, 2012

Mheshimiwa Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa akitoa mchango wake kuchangia ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike kupitia kampeni ya Elimu yao Wajibu wetu, kampeni inayoendeshwa na mabalozi wa Mamlaka ya Elimu (TEA).
**********
Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.

Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.

Mabalozi hao wamefika bungeni na baada ya kutambulishwa wameendelea na zoezi la kuchangisha fedha kutoka kwawabunge wa bunge hilo.
Mratibu  wa kampeni ya Elimu yao Jukumu letu Rebeca Gyumi  akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda  jinsi harambee ya uchangiaji mabweni inavyoendeshwa na makusudio ya harambee hii. TEA inakusudia kuchangisha jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 2.3 zitakazotumika kujengea hosteli 30 katika mikoa minane nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii na Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mh. Margreth Sitta akitoa mchango wake kwa TEA katika kuchangia harakati za Mamlaka ya Elimu Tanzania kuhakikisha wanafunzi wa kike wanakuwa na makazi salama.
Mheshimiwa Vicky Kamata (MB)(Katikati) akijaribu moja ya huduma ya kuchangia kampeni hii ya ujenzi wa mabweni  kulia kwake ni Nancy Sumari Miss Tanzania 2005 na kulia kwake ni Faraja Nyalandu Miss Tanzania 2006 ambao ni mabalozi wa kampeni hii.
Mh. Sophia Simba Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na Watoto akitoa mchango wake kuchangia kampeni hii bungeni. Ili kuchangia pia unaweza kutuma neno CHANGIA TOFALI kwenda namba 15564 ambapo utakatwa shilingi 250 tu za kitanzania.
Mbunge wa Kilosa Mh. Mustapha Mkulo (MB) akitoa mchango wake kuchangia kampeni hii. Mabalozi wa harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za watoto wa kike  waliamua kwenda bungeni kuwaomba wabunge wachangie kampeni hiyo.
Posted by MROKI On Monday, August 13, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo