October 26, 2011

"Saa Ishirini na Nne" Hotuba ya Nyerere 27 Machi, 1979 dhidi ya Gadafi

Mwaka 1979 Mwalimu, Julius Nyerere aliwahutubia wananchi juu ya Ujumbe wa Gadafi uliotumwa kwake wakati Tanzania ikiwa katika vita dhidi ya Uganda. Hotuba ile ilipachikwa jina Saa Ishirini na Nne na hii nikutokana na kwamba Kanali Gadafi wakati huo alikuwa akitaka kuisaidia Uganda katika mgogoro huo. Gadafi aliipa Tanzania Saa 24 kuwa imetoa majeshi yake katika ardhi ya Uganda lakini Tanzania haikufanya hivyo na Nyerere alimjibu Balozi wa Libya aliyetumwa na Gadafi amfikishie Gadafi hayo maneno. Nyerere aliweka wazi nini alimjibu Gadafi, soma hapa. 




1 comment:

  1. Na baadhi ya Watanzania wanasahau haya aliyotufanyia huyu Gadafi, ilipaswa tukawasaidie Walibya kumng'oa

    ReplyDelete