Nafasi Ya Matangazo

April 10, 2024



Na Emmanuel Amas, Singida
Watu saba wamepoteza maisha na wengine nane wamejeruhiwa baada ya basi ya kampuni ya Lujiga lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga lori kwa nyuma katika kijiji cha Malendi kilichoko katika tarafa ya Shelui wilayani Iramba mkoani Singida.
 
Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida ,Pipi Kayumba amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 alfajiri baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kumudu basi hilo na kugonga lori lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara.
 
Inadaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo uzembe wa dereva wa basi la Lujiga ambae alishindwa kuona lori hilo kutokana na ukungu na mvua iliyokuwa ikinyesha muda huo.
 
Majeruhi wa ajali hiyo Wanatibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida na Hospitali za wilaya ya Iramba na Igunga.
 
Dereva wa basi hilo la Lugiga Express ametoroka baada ya ajali hiyo kutokea kwa ajali hiyo na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.

Posted by MROKI On Wednesday, April 10, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo