Nafasi Ya Matangazo

December 09, 2022


Zahanati ya Baga ni moja ya Zahanati zinazopatikana katika Wilaya ya Morogoro vijijini, kwenye safu za mlima Uluguru. 

MSD katika jukumu lake la kusambaza dawa kwa wateja kiutaratibu hufikisha dawa hizo moja kwa moja hadi kituo husika na kufanya makabidhiano mbele ya Kamati ya afya ya eneo husika.

Gari ya MSD lililazimika kupanda Mlima Uluguru na katikati ya safari wananchi walitoa ushirikiano kusaidia  kuzisogeza bidhaa hizo kwa kutumia pikipiki kwani hakuna barabara ya magari eneo hilo, zaidi ya njia ya watembea kwa miguu na pikipiki tu.

Hata baada ya kusafirishwa na pikipiki bidhaa hizo zilivushwa mtoni kwenda upande wa pili ilipo zahanati ya Baga,na ndipo makabidhiano yakaendelea.

Muuguzi Mkuu wa Zahanati ya Baga Sara Manyagi ameishukuru MSD kwa kuhakikisha bidhaa  za afya wanazoomba zinapatikana za kutosha na kwa wakati pamoja na changamoto za kijiografia.

Posted by MROKI On Friday, December 09, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo