Taarifa hiyo imewasilishwa kwa Waziri Jafo
ofisini kwake jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu
usafishaji wa Mito na Mabonde Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Mshote.
Hivi karibuni alifanya ziara ya kikazi ya kukagua mto huo katika Kata ya Mogo Mtaa wa
Kipawa baada ya kupokea malalamiko kuhusiana na athari za kimazingira
zinazotokana na usafishaji wa mto huo.
Hata
hivyo, wakati wa ziara hiyo baada ya kusikiliza maoni ya wananchi alipata maoni
yanayokinzana ambapo wengine walidai shughuli za usafishaji mto huo zimeleta
athari kwa mazingira na wengine wakidai zimeleta manufaa makubwa kwa jamii
inayozunguka eneo hilo.
Itakumbukwa Februari 2021
Waziri Jafo alikutana na wadau wanaojishughulisha na uchimbaji mchanga katika
mkoa huo kujadili changamoto za kimazingira zinazotokana na uchimbaji mchanga
kiholela kiholela katika mito na mabonde ili kuweka utaratibu mzuri.
Kikao hicho kiliwezesha
kuandaliwa Mwongozo wa usafishaji mito utakaotumika katika Mkoa wa Dar es
Salaam kwa lengo la kuondoa mchanga, taka ngumu na tope ili kupunguza au
kuondoa madhara ya mafuriko ambao ulitolewa kwa mujibu wa kifungu cha 57 (2)
cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004.







0 comments:
Post a Comment