March 21, 2012

Rais Kikwete awasili Iringa kufunga Wiki ya Maji kitaifa

 Rais Jakaya Kikwete leo amewasili Mkoani Iringa na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama, dini na Serikali katika uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa. Pichani Rais Kikwete akisalimiana na Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji w Makampuni ya ASAS, Salim ‘Asas’ Abri muda mfupi baada ya kuwasili mjini Iringa.
 Rais Jakaya Kikwete (katikati) akizungumza jambo wakati wa mapokezi yake muda mfupi baada ya kuwasili mkoani Iringa hii leo tayari kwa kufunga maadhimisho ya wiki ya Maji kesho katika uwanja wa Samora. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Deo Sanga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Cristine Ishengoma na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge.
 Rais Jakaya Kikwete akingalia burudani ya ngoma katika uwanja huo wa Nduli.
Rais Jakaya Kiwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Majembe, Sett Motto.

No comments:

Post a Comment