March 21, 2012

Naibu Waziri wa Maji azindua mradi wa uvunaji maji ya Mvua Iringa

 Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge akiweka jiwe la msingu kuzindua rasmi ujenzi wa mradi wa maji uliozaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia mradi wake wa EABL Foundation leo katika Hospitali ya Frelimo ya Manispaa ya Iringa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maji duniani itakayoadhimishwa tarehe 22 Machi 2012.Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda na Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Teresia Mhongwe. Zaidi ya watu wapatao 150,0000 wanaohudumiwa na hospitali hiyo watanufaika.

Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda, akizungumza mara baada ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge  kuzindua Mradi wa uvunaji wa maji ya mvua.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda, akimwelezea Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge  juu  ya mradi wa uvunaji wa maji ya mvua.Kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Stellah Kiwele.

Baadhi ya wauguzi wa Hopitali hiyo ya Wilaya ya Frelimo wakitoka eneo la mradi.
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda (katikati)  akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa,Teresia Mhongwe.

No comments:

Post a Comment