Nafasi Ya Matangazo

March 31, 2011

 Mkazi wa Kichangani ndani ya Manispaa ya mji Kasoro Bahari Morogoro, Fatma Senga ambaye nae amefuata nyayo za babu wa Loliondo, Kaka wa Mbeya , Dada wa Tabora na hivi sasa ni yeye Mama wa Kichangani Morogoro anayetoa dozi ya kipimo cha kikombe/Glasi.

Huyu yeye hana kipimo maalum na vikombe vyake kwa jinsi vilivyoonekana ni vile vidogo vya Chai na Bilauri za bati.

Mama huyu nadai kuoteshwa na Mungu usiku wa kuamkia Machi 30 na leo ameanza kugawa dozi hiyo kwa gharama za sh. 200 tu kwa kipimo.

Mapema leo Mkuu wa Wilaya ya ya Morogoro, Said Mwambungu pamoja na maofisa wa wilaya akiwepo Mkaganga Mkuu wa Wilaya walifika nyumbani kwa mama huyo na kumwomba daktari achukue sampuli ya dawa hiyo kwa uchunguzi kujua usalama wake.

Zaidi ya watu 200 wanasadikiwa kupata huduma hiyo kwa siku mbili zilizopita.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu akizungumza jambo baada ya kutembelea eneo hilo la Kichangani na kuzungumza na Mama Fatma juu ya tiba yake na kumpa mwongozo wa kufanya shughjuli hiyo bila kuleta usumbufu wala madhara kwake na jamii itakayotumia tiba hiyo.
 
Mwambungu aliambatana na viongozi kadha wa ofisi yake baada ya kupata taarifa ya kuwapo kwa KIKOMBE katika Wilaya yake.
Hivi ndo Vikombe, Glasi na Bilauri zinazotumika kugawa dozi ya kutibu magonjwa mbalimbali yakiwapo yale sugu yaliyoshindikana kwa dawa za kisomi.

Aidha Mama fatma yeye alikuwa ni mtoa tiba Mbada tabgu mwanzoni mwa miaka ya tisini hadi hapo alipoooteshwa na Mungu.

Haya Watanzania huenda ndo yale mambo ya unabii yanayo semwa katika vitabu vitakatifu kuwa nyakati za mwisho.
Posted by MROKI On Thursday, March 31, 2011 No comments
 Meneja Mahusiano wa TBL,Edith Mushi (pili kushoto) akipeana mkono na Afisa Uhusiano wa UMIVITA,Tungi Mwanjala (tatu kulia) wakati wakati wa kukabidhi msaada wa Shilingi 2.5 Mil, kwa ajili ya ukarabati wa jengo la ofisi ya Chama cha Umoja wa Miradi ya Viziwi Tanzania (UMIVITA) iliyopo ndani ya Shule ya Viziwi Buguruni leo.wengine pichani ni Mkurugenzi wa Chama cha Kuhudumia Viziwi Tanzania,Matirda Ngonyani (kulia),Katibu Mtendaji,Rahim Othman pamoja na Judith Robert kutoka chama cha kusaidia Viziwi la TANZANEAR.
Jengo linalotakiwa kukarabatiwa na fungu hilo la fedha.
Posted by MROKI On Thursday, March 31, 2011 No comments
Maisha yanakwenda .....
Posted by MROKI On Thursday, March 31, 2011 No comments

March 30, 2011

 Naibu Waziri wa Mawasiliano sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga na Ofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Clarence Ichwekereza wakimiskiliza Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor,walipotembelea Ofisi za Airtel Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga akizungumza mara baada ya kutembelea ofisi za Airtel Dar es Salaam leo kujioneaa shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo ya simu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sam Elangalloor.
Posted by MROKI On Wednesday, March 30, 2011 No comments
   Mkuu wa wilaya ya Urambo Anna Magowa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa madarasa mawili yaliyojengwa  kwa ajili ya shule ya sekondari ya Kaliua iliyopo Wilaya ya urambo Mkoani Tabora, anaeshudia ni Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule, Madarasa hayo yalijengwa kwa thamani ya shilingi milioni 30.
Meneja wa mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom(Vodacom Foundation)Yessaya Mwakifulefule akiwasaidia kufanya usafi  baadhi ya wanafunzi wa shule ya secondary ya Kaliua iliyopo Wilaya ya urambo Mkoani Tabora mara baada ya kufika  shuleni hapo kwa lengo la kukabidhi madarasa mawili yaliyojengwa na mfuko huo kwa thamani ya shilingi Milioni 30.
Posted by MROKI On Wednesday, March 30, 2011 No comments
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya picha yake iliyochorwa kutoka kwa Naibu Waziri wa maji, Gerryson Lwange (wapili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Lwange Ofisni kwake jijini Dar es salaam Machi 30.2011. Zawadi hiyo imetolewa na watumishi wa Wizara ya Maji.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maji baada ya kukabidhiwa zawadi ya picha yake iliyochorwa, ofisini kwake jijini Dar es salaam.  Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Jerryson Lwange akifuatiwa na katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Sayi. 
Posted by MROKI On Wednesday, March 30, 2011 No comments
 Makamu wa  Rais  Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiagana na Wanafunzi wa Shule ya sekondari Felix Mrema Daraja la pili baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Ghorofa la Shule hiyo ambapo ameahidi kuchangia shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi huo. Makamu wa Rais amekamilisha ziara yake ya siku nne ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo.
Mzee wa kabila la Muarusha katika kijiji cha Terrat Nadosollo Wilayani Arusha Saigura Loilola, akimvisha vazi la Mgolole la Heshima na Uongozi wa kabila la Muarusha (Masai)  Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipowasili kwenye uwanja wa Terrat Nadosollo Wilayani Arusha kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara. Makamu wa Rais amekamilisha ziara yake ya siku nne ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoni Arusha leo.
Posted by MROKI On Wednesday, March 30, 2011 No comments
OPEN LETTER TO JOHN MASHAKA,

TANZANIA IS NOT IN FINANCIAL CRISIS DEBATE

I believe there's no Financial Crisis in Tanzania but we have plenty of opportunities.. Wadau someni na niambie msimamo wenu..

We Tanzanians need to solve the obvious. We have resources that we are not exporting - Coffee, Beer, Wine, tea, bananas and also Culture. We don't need a genius to solve problems in Tanzania. We need people to start with themselves and make changes they want to see in the country.The idea of a white man or an angel that will come to Tanzania to give us riches is stupid and ignorant.USA wapo watu kibao ambao ni broke.. first there's no country with so much dept like USA. So if its financial crisis .. its in USA and not Tanzania.

Tanzania does not have financial crisis but it lacks motivation and also resource exploration due to corruption and uneducated population. I spent over 10 month in Tanzania and saw the lack of sense of urgency in everything.. Except drinking beers and nyama choma.As Tanzanians , we need to expand our market and create demand for our goods globally. That is what china did and you can see the proof in your life. Imagine if Tanzanian Beers , tea. wine, shoes, fruits and other goods were sold to Germany, USA, African Countries and Europe. Only this will create employment in Tanzania and raise the income of many Tanzania.

Most Tanzanians leaders don't realize is how foreign companies are killing our goods and markets. When Sabmiller from South Africa buys TBL and Konyagi , it means hunger and poverty to Tanzanians. TBL can't sale to Europe any more and SAB Miller is also making sure SAFARI BEER STAYS IN TANZANIA and never to reach larger markets. This system creates a non growth within our economy. How many cigarrates or Beers can Tanzanians buy in Tanzania?? Not much.. If they do then they will become unproductive citizens.

Foreign companies buying Tanzanian Industries are doing so to kill our goods and making sure our produce (Goods) will never reach their market.Now , since there's a number and market limit , Tanzanians can't get more jobs or increase exports due to lack of foreign market. What we need to do as Tanzanians is to make sure we take control of our Foreign market and at the same time be the ones in our local market educating farmers and industries on how to produce high quality goods for export.Only a Tanzanian can sale Tanzania in foreign Market and at the same time benefit producers at home.

You see Chinese and other foreigners selling their home goods in Tanzania.. RIGHT??? Then the same should happened to Tanzanians who have the opportunity to be abroad..KAMA WEWE UNAPIGA SIASA.. then TALK IS CHEAP. Put your money up and let's work to help the people. There's a lot of Tanzanians abroad working and getting used up without even remembering where they come from. If you in USA, Germany or Italy and you have people .. I mean your people suffering then it doesn't make any sense for you to say or write. You want to make a change? Then start doing and stop acting.

South Africans are buying up cashews from Tanzania and processing it in capetown. What happened after that ?? It's in the stores in here in Los Angeles as Cashews from South Africa.Do you know how much is Zebra skin?? $1700

WHAT BOUT POUND OF COFFEE $ 3 Ok, I believe it's not the leaders.. We need to make the changes and start leading our people to the right channels. Remember, WAKOLONI and many now are able to cheat us in Tanzania because many people don't know how the system works in foreign countries.

President Kikwete and Govt need to use Tanzanians abroad as resources and tools so that we can help local markets.

Who can represent Tanzanians farmers in USA better than Mashaka?? Or any other Tanzanians abroad.Tanzania Gov't must think and act like USA and China. They use their citizens and businesses to open up market for the entire country.Imagine if Tanzania Govt helped and provided resources to locally owned businesses to sale in foreign markets.. SERENGETI , KILIMANJARO BEERS WOULD BE AVAILABLE WORLDWIDE.

I exported Konyagi to USA.. Baadae. Hata kiwanda wamekuja kuwauzia makaburu.. I can't say it is Tanzanian Drink now..Already mistakes has happened and most of the industries in Tanzania no longer belong to Tanzanians

We have to get the local produce and also work with our farmers , miners and also our brothers and sisters in Tanzania so that we can open market for them abroad.Then Tanzania will start getting dollar income and things will start changing before our very eyes.We can't be the only consumers and producers at the same time and expect to grow.

Where is the purchasing power going to come from ??Tanzanians are flooded with trash from the foreign industries and this is an example of what we need to do with our own economy and market. We have to flood foreign markets with Tanzanian goods.It's very simple and it does not take PHD or the Europeans to tell us what to do. Let's work on the obvious and we can make progress. Can you imagine??? TANZANIA IS ALLOWING TOOTH PICKS FROM CHINA TO BE SOLD AND IMPORTED IN TANZANIA???WHAT ABOUT ORANGE and APPLE JUICE?

It's not smart but it's not the Govt fault but our own.NAFIKIRI WABEBA MABOKSI WAANGALIE TENA KWANINI WANABEBA BOKSI.. LABDA WACHUNGULIE NDANI YA MABOKSI .

It's funny.. Majority of Tanzanians abroad don't even have proper immigration paperwork.. But this is another issue.

But it does relate to the economy and also affect Tanzania human capital productivity. When a Doctor , Prof, msomi or Eng can't return home due to papers.. it affects his or her decisions in Economic development at home. He or she can not invest in Tanzania since hawezi kurudi na ndugu amewatupa. In return he makes money in USA and nothing goes back to TZ to improve lives.Most people don't know this.. lakini michuzi don't delete this ..

If you work in USA illegally until you reach your retirement age.. You won't be able to collect any social security or retirement income. Not only that..You will be shocked to be charged with Employment Fraud. If you are terminated from your Job, you wont be able to collect Unemployment or insurance during work injury. Wabeba maboski.. I love you... but you have to be aware anytime bomu can bust.. JE UTAKUWA TAYARI??? Mashaka and all the people are great.. we need to push forward and get it in where we can..Nilikua hapo Tanzania since January til sept 2010.. Nimeona mengi. Kwanza hakuna Financial Crisis..

Mashaka You are extremely brilliant and smart but brother.. Tanzanian economy can not be judged by bank reports or financial institutions alone. There's many people in rural areas with Dairy Farms, Fisher men's, miners and farmers whose income is not reported. FINANCIAL CRISIS?? NO. Tanzania economy is not based on credit lines or wall street compared to USA. Majority of Tanzanians are using cash for their purchases. If you compare Tanzanian teacher and American Teacher.. I can say American Teacher is broke and also in debt.

Currently, USA is in debt..

Average.. every american (Debt per citizen is $178,444) and Spending Ratio to GDP is 45.6451487%)

An average savings per American family is $7,964..You have to look at the economics now.. Let's go

USA POPULATION 311 MILLION. US TAX PAYERS 111 MILLION. UNEMPLOYED Officially 15, MILLION

ACTUAL UNEMPLOYED 26 MILLION. 43 MILLION ON GOVT ASSISTANCE (FOOD STAMPS).

54 MILLION RETIRED.BANKRUPT - 1 .6 MILLION JUST THIS YEAR.Now there's no land in America that's free or mines you can explore.. Now can you compare that to Tanzania? We are the ones with everything going right.. THAT'S WHY YOU SEE CHINA MAN IN TANZANIA.OR USA now trying to open trade with Tanzania..

Even turkey and Brazil are coming.. What are they after?? Now we Tanzanians must be alert and also fast to grab our own opportunities before Foreigners. Do you know most apple fruits sold in Tanzania come from South Africa?? Yes and they are delivered fresh by plane.. What about our bananas?? Can't we fly them to Saudi??


Mdau Los Angeles
Julius Temu
Julius Imports and Exports Limited
Mobile: 323-594-6205

Posted by MROKI On Wednesday, March 30, 2011 No comments

March 29, 2011





 As a sister company of ZG-Designs that has a large base for marketing in Tanzania, ZG Films presents Zanzibar's first high quality Bongo Movie, Glamour produced by Javed Jafferji and Directed by Amitabh Aurora which tells the story of young Zanzibari girl who dreams of becoming a model and her trials and tribulations as she leaves her conservative Muslim home to peruse her glamorous new career in the big city, Dar es salaam.

Staring one of Tanzania's top models, Eva Issac, and celebrated Tanzania couturier, Mustafa Hassanali, this is the film that will undoubtedly appeal to the masses in a country filled with beauty pageants and where becoming a model is a dream of many - both male and female.Glamour,a Swahili Bongo Film with English subtitles is set to be released across the nation this April.


Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Ujumbe wa Waandishi wa Habari kutoka  India ,  Ofisini kwake jijini Dar es salaam  Machi 29,2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na kiongozi wa Ujumbe wa Waandishi wa Habari kutoka  India , Bibi Indrani  Begchi, Ofisini kwake jijini Dar es salaam  Machi 29,2011.  Kushoto ni Balozi wa India , K. V.  Bhagirath
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
Baada ya kuanza kwa tiba ya KIKOMBE cha Babu wa Loliondo, Mangi wa Tarakea na Dogo wa Mbeya hivi sasa ameibuka mwanamke mwingine akidai kutoa tiba ya namna hiyo huko Tabora na huyu sasa anajulikana kama Dada.

Mwana dada aliye ibuka Tabora anakwenda kwa jina la Margareth Mutalemwa na tayari ameshaanza kukusanya umati mkubwa wa wtu katika makazi yake kama picha zinavyoonekana hapo juu.
Taarifa zaidi ingia HAPA kwa Mdau Mkala Fun
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
 Hii ilikuwa leo mchana pale Posta karibu na NBC Club mgambo wa Manispaa ya Ilala walipomkwida mvuja jasho huyu kwa kosa la kuuza nguo mtaani.
 Walimvamia kundo mithili ya jamabazi aliye na silaha kali....
 Baadhi ya nguo zake...
Hapa alifikishwa kwa mkuu wao kujibu tuhuma.
Licha ya kuwa wachuuzi hawa wanachafua mandhari ya jiji saaaafi la Dar e Salaam lakini Mgambo hawa wamekuwa ni wanyanyasaji wakuwa wa vijana hawa walio amua kijitafua ridhiki na kukwepa kazi za ukabaji na uporaji.

USHAURI
Ni vyema Mgambo hawa wakatafuta kazi nyingine ya kufanya kama vile kufuatilia watu wanao chafua mji kwa kutupa taka hovyo na kukusanya faini hizo. Mfano mzuri ni katika jiji la Mwanza na Manispaa ya Moshi.

Mgambo hawa watakuwa wanamanufaa zaidi na wengi tutawaona wa maana wakisimamia usafi wa jiji na si kukamata masufuria ya mamalishe na mitumba ya machinga.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
 
 
 
Hii ndo bei ya soko leo kwa baadhi tu ya maduka ya kubadilishia fedha katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya akiwaeleza  wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) kuhusu mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa 2010 wakati wa mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mzuri Issa ambaye ni mratibu wa TAMWA Zanzibar na kushoto ni Gladness Munuo.
 Gladness Munuo na Nasima Haji Chumu ambao ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakikata keki kwa niaba ya wenzao huku wanachama wengine wakishuhudia  mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa  wakati wa  mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
 Palikua kweupe namna hii sehemu ya kupokelea abiria/wageni....
 Baada ya muda wapokeaji walianza kufika...
Wakajaaa hivi...
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
 
 
Dereva wa gari hili alinisukuma sana kumpiga picha yeye na gari analo endesha kutokana na ukubwa wa gari na umri au umbo la dereva huyu anaeonekana anasura ya kitoto. 
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
Mwendesha pikipiki mkazi wa Jiji Dar es Salaam akiwa ameweka kati na Polisi wa doria ya Pikipiki maarufu kama Tigo, karibu na duka la Shprite Kamata leo. Mtu huyu baadae aliachiwa na askari hawa baada ya kubaini kuwa wamepigwa picha na kumfuata mpiga picha kujua sababu ya kupigwa picha na kujibiwa kuwa
"WATU WAPO KAZINI WASIWE NA SHAKA"
wakaamua kuondoka.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
 
Tangu kutokea kwa milpuko ya kigaidi katika nchini Septemba 11, 1998 kulipelekea baadhi ya sehemu nyeti kuwekwa katika hali ya usalam ikiwapo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam ambapo awali wananchi walikuwa wakiruhusiwa kupanda sehemu ya juu ya jengo la uwanja huo na kuangalia ndege zikitua na kuruka. Hivi sasa amri nyingine imewekwa katika eneo hilo la kukataza hata watu waliokuwa wakikaa katika ngazi hizi juu kukaa na iwapo ukikamatwa utachukuliwa hatua kali.

Baadhi ya wananchi wanasema hali hiyoinasababishwa na uvivu wa maofis usalama uwanjani hapo kushindwa kuwakagua watu na kuwaruhusu kupanda huko na kujionea mandhari ya uwanja wao wa ndege wa Kimataifa.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
 
N0 PARKING.....Mfanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam akipaka rangu katika maandishi ya kuzuia magari kuegesha karibu na uwanja huo leo.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 1 comment
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (shoto) pamoja na Mwakilishi wa Nakayama kutoka Japan ambae pia ni Rais.wa Shirikisho la Uchumi na Maendeleo kwa nchi za Africa(AFRECO) Seneta Tetsuro Yamo (kulia) wakiwa katika moja ya darasa la shule ya Sekondari ya Nyamisati wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Machi 28,2011.
 Mama Salma Kikwete (kulia) akimtambulisha mgeni wake Machi 28.2011 Seneta Yamo shuleni hapo.
 Hapa ilikua ni kuonesha ishara ya mshikamano katika kuleta maendeleo kwa watoto wa kike.
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama wakimsikiliza kwa makini mgeni wao ambae hayupo pichani alipozungumza nao Machi 28.2011 alipowatembelea na kuangalia maendeleo ya shuleni hapo.
 Picha ya pamoja ilipigwa kati ya uongozi wa shule, wanafunzi na wageni.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa pamoja na Mgeni wake kutoka Japan Seneta Tetsuro Yamo (kulia mwenye tai nyeusi) wakikagua majengo ya shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA wilayani Rufiji mkoa Pwani (Machi 28,2011) kuangalia maendeleo ya shuleni hapo.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments
  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo