Nafasi Ya Matangazo

September 28, 2022

Mnyama Simba ameelezwa ndiye anayevutia idadi kubwa ya watalii wanaoitembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha inayotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha wanyama hao nchini na kwa bara zima la Afrika.Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa sambamba na watendaji na Maafisa Tarafa wa Wilaya ya Irimga pamoja na kiongozi wa hoteli ya Jabali Asili wakati wa ziara ya kitalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
Mnyama Simba ameelezwa ndiye anayevutia idadi kubwa ya watalii wanaoitembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha inayotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha wanyama hao nchini na kwa bara zima la Afrika.Mnyama Simba ameelezwa ndiye anayevutia idadi kubwa ya watalii wanaoitembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha inayotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha wanyama hao nchini na kwa bara zima la Afrika.


Na Fredy Mgunda, Iringa
MNYAMA Simba ameelezwa ndiye anayevutia idadi kubwa ya watalii wanaoitembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha inayotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha wanyama hao nchini na kwa bara zima la Afrika.

Wakizungumza wakati wa ziara ya Utalii ya maafisa Tarafa na Watendaji kutoka wilaya ya Iringa iliyoratibiwa na mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo, walisema kuwa wamefurahishwa na namna hifadhi hiyo ilivyokuwa na vivutio vingi ambavyo vipo ndani ya hifadhi hiyo kama vile mnyama Simba.

Stella makali na Aunt Mbilinyi ni watendaji wa kata walisema kuwa wamefurahi kufanya utalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya kuona namna ambavyo mnyama Simba anavyofanya mapenzi jambo ambalo.

hawajawahi kuliona toka wanzaliwe hivyo inawafanya watafute muda mwingine wa kwenda kufanya utalii katika hifadhi hiyo.
 
Walisema kuwa wamefurahia kutembelea hifadhi hiyo kwa namna ambavyo wameona wanyama Simba anavutia kiasi kwamba ukiwa katika hifadhi hiyo utakuwa na furaha muda wote kwa namna ambavyo vivutio vingi vilivyopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
 
“Tumerithishwa,Tuwarithishe tuungane kwa pamoja kuokomeza ujangili katika hifadhi yetu ya Ruaha iliyopo mkoa wa Iringa ili hata watoe watu waje waone wanyama na vivutio vilivyomo hifadhini”alisema makali
 
Emmanuel Ngabuji ni kaimu Afisa Tarafa Pawaga alisema kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha imejaliwa kuwa na vivutio vingi ambavyo mtalii akifika katika hifadhi hiyo atafurahia na hatatamani kuongoka kutoka kuwapata furaha awepo kwenye hifadhi hiyo ikiwa na kumuona mnayama Simba ambaye amekuwa kivutio kikubwa.
 
Ngabuji alisema kuwa watendaji wengi imekuwa mara yao ya kwanza kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kumshuhudia mnyama Simba akiwa katika fungate jambo ambalo liliwafurahisha watalii wote walikuwepo katika hifadhi hiyo ya taifa.

Simba ni mnyama anayependwa katika historia yake yote, na ni ishara ya ujasiri na nguvu. Wanyama hawa kitabia wana miili yenye nguvu—na miungurumo inayoweza kusikika kutoka umbali wa maili tano,” alisema.

Ngabuji alisema kuwa wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akiutangaza utalii wa ndani kupitia filamu ya Royal Tour ambayo imeanza kuleta matokeo chanya ya ongezeko la watalii nchi na watalii wa ndani kuongezeka kutembelea vivutio  mbalimbali.
 

Naye Menaja Msaidizi wa Hoteli ya Jabali Asili, Josina Mkundi alisema; “Filamu ya Royal tuwa imewaongezea wageni wengi wa kimataifa wanaotembelea hifadhi hiyo na kujionea vivutio vyake lukuki, akiwemo mnyama Simba. Navyoongea sasa hoteli yetu imejaa.”

“Tuna wageni wengi kutoka Uingereza, Ujerumani na Marekani. Pamoja na kufurahia manzari nzuri ya hifadhi hii, wanyama wakubwa na wadogo na aina mbalimbali za ndege, mnyama wanayetaka kumuona zaidi na bila kuchoka ni Simba.”

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa lengo la kuwapeleka maafisa Tarafa na watendaji kutalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni kutambua umuhimu wa utalii na namna ambavyo wanaweza kuwalinda wanyama pori wasitoweke ili kuwaliaisha wananchi wengine. 

Moyo alisema kuwa maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha kunaongeza chachu ya ongezeko la watalii katika ukanda wa nyanda za juu kusini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kusisimua uchumi kupitia sekta hiyo muhimu nchini. 

Alisema kuwa mnyama Simba amekuwa kivutio kikubwa kwa watalii ndio maana mtalii asipoona Simba anahisi kama hajafanya utalii, “leo maafisa Tarafa na watendaji wamefanikiwa kumuona Mnyama Simba akiwa fungate jambo ambali limefurahisha sana”. 

Mohamed Moyo alisema barabara hiyo itajengwa kupitia sehemu ya mkopo wa masharti nafuu wa Sh Trilioni 1.2 uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha usalama, ustahimilivu wa tabianchi, uwezo wa barabara za ndani na viwanja vya ndege vya mikoa.

Mmoja wa watalii hao kutoka Ujerumani, Romy Wagner alisema mbali na kushuhudia kwa macho yake aina mbalimbali za wanyama na uoto wa asili hifadhini humo, shauku yao ilikuwa kuwaona Simba kwa macho yaolakini pia waliona chui saba wakiwa katika kundi moja, juu ya mti. 

Naye dereva wa mkuu wa wilaya ya Iringa Ramadhan Sosovele alisema makundi makubwa ya nyati, tembo na simba yalikua kivutio chao kikubwa na akafichua kwamba watendaji na maafisa tarafa wengi wao ni mara yao ya kwanza kuwaona wanyama hao katika maisha yao ya asili hifadhini tofauti na walivyozoea kuwaangalia katika filamu.

Posted by MROKI On Wednesday, September 28, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo