Nafasi Ya Matangazo

September 29, 2022

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habariWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Msonde kufuatilia Malalamiko na changamoto zote zinazowakabili Walimu wa Ajira Mpya 9,800 ili ziweze kufanyiwa kazi.

Eliud Rwechungura - Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amemwagiza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Msonde kufuatilia Malalamiko na changamoto zote zinazowakabili Walimu wa Ajira Mpya 9,800 ili ziweze kufanyiwa kazi.

Ametoa maagizo hayo Septemba 28, 2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kuagiza kufuatiliwa Malalamiko yote ambayo amekuwa akipokea kutoka wa Walimu wa Ajira Mpya zilizotolewa na Serikali mwezi Juni, 2022.

Bashungwa amesema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa Walimu wa Ajira Mpya ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa baadhi ya wilaya ambazo hazijatoa fedha za kujikimu kwa Walimu hao.

Aidha, Bashungwa ameagiza kutolewa kwa ufafanuzi wa viwango vya malipo kwa mujibu wa tararibu na vigezo vinavyotumika katika malipo hayo ili kuondoa sintofahamu ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.

Bashungwa amesema Serikali ya awamu ya sita ni sikivu na itaendelea kusikiliza na kutatua changamoto watakazokumbana nazo Wakati wakitekeleza Majukumu ya kuwafundisha wanafunzi.

Ikumbukwe kuwa tarehe 26 Juni, 2022 Seikali ilitoa ajira za kada za ualimu kwa waombaji wenye sifa waliokidhi vigezo 9,800 ambapo walimu 5,000 wamepangwa shule za Msingi na walimu 4,800  shule za sekondari.

Posted by MROKI On Thursday, September 29, 2022 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo