Nafasi Ya Matangazo

July 27, 2020

Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mh. Balizi Omari Ramadhani Mapuri akifungua semina ya siku tatu ya waratibu wa Uchaguzi, wasimamizi, wasimamizi wasaidizi na maafisa Uchaguzi kutoka Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida inayofanyika Jijini Dodoma. 
Balizi Omari Ramadhani Mapuri alisema, wasimamizi hao wa uchaguzi katika Kanda ya Kati wanatakiwa kuzingatia maadili wanapofanya kazi hiyo. Mafunzo ya siku tatu jijini hapa yaliyokutanisha washiriki 162, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mh. 
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mgeni Rasmi
Maafisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi.
Washiriki wakijaza fomu maalum kabla ya kula kiapo mbele ya Hakimu.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi Wilaya ya Dodoma, Mary Senapee akiwaongoza wasimamizi wa uchaguzi Mkuu kutoka kanda ya Kati kula kiapo.
Washiriki wote ambao ni waratibu Uchaguzi, Wasimamizi, Wasimamizi wasaidizi na maafisa uchaguzi wakila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi Wilaya ya Dodoma, Mary Senapee.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu kuzingatia weledi na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili kupunguza au kuondoa kabisa malalamiko yanayoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi.

Akifungua Mafunzo ya siku tatu jijini hapa yaliyokutanisha washiriki 162, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mh. Balizi Omari Ramadhani Mapuri alisema, wasimamizi hao wa uchaguzi katika kanda ya Kati wanatakiwa kuzingatia maadili wanapofanya kazi hiyo.

Alisema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko.

Balozi Mapuri alisema wasimamizi hao, katika mkutano huo wa siku tatu (3) wanatakiwa kubadilishana uzoefu, kujadili namna bora ya kufanikisha uchaguzi, lakini pia kujadili namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika hatua mbalimbali za uchaguzi.

Aidha Balozi Mapuri, aliwataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa kufuata maadili kwa kuzingatia Sheria, Kanuni pamoja na maagizo na maelekezo yanayotolewa na Tume ya  Uchaguzi.

“Mnatakiwa kutumia mkutano huu, kubadilisha uzoefu na kufanya kazi kwa kufuata maadili kwa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo pamoja na maagizo ya Tume ya uchaguzi,” alisema.

Balozi Mapuri alisema wasimamizi hao wameaminiwa na kuteuliwa na Tume katika nafasi hizo za usimamizi wa uchaguzi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo wanatakiwa wajiamini na kujitambua.

Alitoa mwito kwa wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi kijiografia na kuhakikisha kwamba wanawatumia vizuri wasaidizi walio chini yao katika maeneo yao ili kutoa matokeo bora.

Pia aliwataka wasimamizi hao kujua miundombinu mbalimbali ya kufika kwenye vituo vya kupigia kura katika majimbo wanayosimamia uchaguzi.

Balozi Mapuri aliwataka washirikishane na vyama vya siasa pamoja na wadau wengine wa uchaguzi katika mstakabali mzima wa uchaguzi ili kuongeza uwazi katika uchaguzi na hivyo kuleta ufanisi.

Kati ya washiriki wa mkutano huo, wasimamizi wa uchaguzi wapo 24,  wasimamizi wasaidizi uchaguzi katika majimbo wapo 87, maafisa uchaguzi  24, waratibu wa uchaguzi watatu na maafisa ugavi 24 ambapo kati yao 55 wanatoka mkoa wa Dodoma, Morogoro 61 na Singida 46.

Katika kwenda kutekeleza kikamilifu majukumu yao usimamizi hao katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu, walikula viapo viwili moja cha kujitoa katika vyama vya siasa na nyingine ya kutunza siri za uchaguzi wanaposimamia uchaguzi.

Kiapo hicho cha utii kiliongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi Wilaya ya Dodoma, Mary Senapee ambaye aliwataka washirikishi hao kusaini baada ya kuapa kwani wakikiuka maadili ya uchaguzi ndicho kitakacho wafunga.

Posted by MROKI On Monday, July 27, 2020 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo