Nafasi Ya Matangazo

December 11, 2019

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitafakari wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua ghala la kuhifadhia korosho Nangurukuru wakati alipofanya ziara Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Sehemu ya wakulima na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama wakati alipofanya ziara Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Pwani na Lindi
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 10 na 11 Disemba 2019 amefanya ziara ya siku moja wilayani Mkuranga katika Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi kukagua hatua zilizofikiwa za malipo ya wakulima wa korosho msimu wa mwaka 2018/2019.

Katika ziara hiyo Waziri Hasunga amebaini baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao jambo ambalo limemshangaza Kwakuwa serikali ilishatoa fedha zote kwa ajili ya kuwalipa wakulima.

Amesema kuwa baada ya ziara ya kikazi katika mkoa wa Pwani, Lindi na Mtwara kubaini kadhia iliyopelekea kutolipwa fedha hizo serikali itachukua hatua za haraka.

“Sikutegemea hata siku moja kwamba eti itafika mpaka mwezi wa 12 wakulima wakiwa hawajalipwa kwakuwa imetokea niwahakikishie wakulima wote ambao walileta korosho zao na zilipokelewa, wote watalipwa” Alisisitiza Mhe Hasunga

Amesema kuwa wapo baadhi ya wakulima ambao wanasema hawajalipwa jambo ambalo sio kweli kwani wanafanya hivyo ili kukwepa madeni waliyokopa.

Kuhusu vibarua waliofanya kazi katika msimu huo wa korosho wa mwaka 2018/2019 Waziri Hasunga amesema kuwa madeni yote halali yatalipwa kwa wakati.

Hata hivyo ameeleza kuwa katika msimu wa mwaka 2019/2020 serikali haitajiingiza kwenye ununuzi wa zao la korosho badala yake imetoa fursa kwa wafanyabiashara kununua korosho.

Sambamba na hayo pia amesema kuwa serikali inaendelea kujipanga vyema ili katika siku za hivi karibuni serikali isipange bei elekezi badala isalie kuwa msimamizi mkuu kuhakikisha haki inatendeka katika biashara hiyo.

Ziara ya siku moja mkoani Pwani imetoa taswira ya muendelezo wa ziara ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ambapo leo tarehe 11 Disemba 2019 amewasili katika mkoa wa Lindi.
Posted by MROKI On Wednesday, December 11, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo