Nafasi Ya Matangazo

December 08, 2019

 KATIBU Mkuu idara kuu ya  maendeleo ya jamii,Dokta John Jingu amevitaka vyuo vya maendeleo ya jamii nchini kutoa elimu ambayo itakuwa ni  nyenzo na silaha ya kupambana na changamoto zilizopo katika jamii na kuweza kuleta matokeo chanja.

 Dakta Jingu aliyasema  wakati alipotembelea chuo  Cha maendeleo ya jamii Monduli Mkoani Arusha ambapo pia ametembelea na kujionea  miradi mbalimbali ya wananchi iliyofanikishwa na chuo hicho kwa kushirikiana na wananchi kupia kitengo cha ujasiamali cha chuoni hapo. . 
Alisema kuwa,kama wizara imekuwa ikisisitiza  vyuo hivyo kuhakikisha wanatoa elimu ambayo itakuwa ni silaha ya utatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii ili uwepo wa vyuo hivyo uweze kutambulika kwa vitendo zaidi.
"unajua unaposema upo chuo unasomea kozi fulani mjue kabisa elimu sio sifa tu ama cheti bali jamii yenyewe inatakiwa ikutambua kwa kazi zako unazozifanya kwani   ndizo  zitaweza kukutambulisha kwa jamii  katika kuhakikisha elimu uliyoipata italeta majibu kwenye matatizo yaliyopo."alisema 

Hata hivyo katibu mkuu huyo alifurahishwa na miradi mbalimbali ya kijamii iliyoanzishwa na chuo hicho ambayo bado wananchi wanaendelea kuitekeleza ambayo imewasaidia Sana kujikwamua kiuchumi  hivyo kukimwagia sifa chuo hicho kwa ubunifu mkubwa wa kuleta mabadiliko katika jamii.
 Naye kaimu Mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Monduli ,Elibariki Ulomi alisema kuwa,wamekuwa wakitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii inayowazunguka ikiwemo ufugaji wa kuku,ng'ombe,ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa Sana kujikwamua kiuchumi.

Alisema kuwa,chuo hicho kimekuwa kikitekeleza kwa vitendo elimu wanayoitoa chuoni hapo ambapo wameweza kuibadili jamii hiyo ya wafugaji kwa kusaidia miradi mbalimbali  ya ujasiriamali  sambamba na  kutoa elimu  namna ya kuhifadhi fedha  zao wenyewe na kuweza kukopeshana.

Wakizungumzia namna walivyonufaika na chuo hicho wanakikundi  cha Tuinuane kilichopo Monduli juu ,walisema kuwa,chuo hicho kimeweza kuwapatia mafunzo mbalimbali namna ya ufugaji bora wa kisasa wa ng'ombe na kuku ambapo wameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mradi huo na kuondokana kuwa tegemezi.
Katibu wa kikundi hicho ,Anna Losiloyi alisema kuwa,kikundi hicho kina jumla ya wanachama 30 ambapo wameweza kuwa na kuku Mia moja na ng'ombe mmoja huku wakijishughulisha na biashara ya kushona shanga pamoja na bangili ambazo wamekuwa wakiwauzia watalii na kuweza kutunisha kikundi chao.

Aidha kikundi hicho kimefika mbali zaidi kwa kumwomba Katibu Mkuu kuwazindulia rasmi kikoba ambacho kitawasaidia kuweka  fedha  zao ili waweze kukopeshana .
Posted by MROKI On Sunday, December 08, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo