Nafasi Ya Matangazo

October 10, 2019

 Afisa Nyuki wa wakala wa huduma za misitu(TSF) wilaya ya Shinyanga,Franael Sumari akionesha asali na nta waliyozalisha mwaka huu

Afisa habari na uenezi wa TFS kanda ya Magharibi,Karimu Solyambingu akionesha mtambo wa kutengeneza Nta katika misitu ya TFS Shinyanga.
Mlinzi ofisi za TFS nzega akionesha baadhi ya mizinga ambayo inaendelea kusambazwa katika wilaya hiyo.
 *************
Na Mwandishi wetu, Arusha
Uzalishaji wa Asali na nta  chini, umeongezeka katika Misitu inayosimamia na Wakala wa huduma za  Misitu Tanzania(TFS) kutokana na kuboresha uhifadhi wa mazingira na  wananchi wengi kupata elimu ya kufuga nyuki.

Afisa Habari na uenezi wa TFS Kanda ya Magharibi, Karimu Solyambingu akizungumza na waandishi wa habari, alisema ongezeko la uzalishaji huo wa asali pia limechangia udhibiti wa uhabifu wa mazingira  katika hifadhi za  misitu unaendelea kufanywa na TFS maeneo mbalimbali nchini.

"katika misitu ya hifadhi inayosimamiwa na TFS kanda ya Magharibi,  katika wilaya za Sikonge, Shinyanga,  Nzega  na hata eneo la Manyoni uzalishaji wa asali na nta umeongezeka sana"alisema

Ramadhani mzirai Meneja wa TSF wilaya ya Shinyanga alisema,uzalishaji wa asali katika misitu ya TFS katika wilaya hiyo, umeongezeka kutoka  kilo 130 mwaka 2017/19 hadi kufikia kilom 700 mwaka 2018/19.

"ongezeko hili halijawahi kutokea katika misitu yetu kwani pia tumepata zaidi ya kilo 15 za nta na tumeweza kuwa na mizinga 140 ambayo inazalisha lakini pia wananchi 264 kutoka vijiji 13 tuliwapa elimu na wanafuga nyuki kisasa"alisema

Bibi nyuki wa  kituo cha TFS wilaya ya Manyoni, Jackline Leshabari alisema alisema  uzalishaji wa asali umeongezeka wilayani Manyoni,kutoka tani  1.7 mwaka 2017/18 hadi kufikia tangi 3.2 mwaka 2018/19.

"ongezeko hilo limetokana pia na kiasi cha mvua cha wastani ambacho kilinyesha msimu uliopita ambacho kiliwezesha nyuki kupata maua kwa wingi na maji kwa ajili ya kutengeneza asali "alisema

Mkuu wa TFS wilaya ya Sikonge, Haji Abdalah alisema  kumekuwepo  na ongezeko kubwa la uzalishaji wa asali katika misitu iliyohifadhiwa katika wilaya hiyo na mwaka 2018/19 hadi kufikia tani 100.

"katika misitu hii sasa kuna zaidi ya wafugaji 1000 wanaendesha ufugaji wa kisasa lakini pia sisi kama TFS tumekuwa tukishirikiana nao katika kuandaa mizinga na kuwapa elimu ya ufugaji nyuki "alisema

Yuda Zebedayo ambaye ni mmoja wa wafugaji wakubwa wa nyuki wilaya ya Sokonge alisema mwaka huu anatarajia kuwa na asali  zaidi ya 120  kutokana na kuwepo msimu mzuri katika misitu ya wilaya hiyo.

Katika wilaya ya Nzega Katibu wa mbunge wa jimbo la Nzega vijijini, Basirio Lazaro alisema uzalishaji wa wilaya hiyo, inaendelea kuongezeka hasa baada ya TFS kuwapa  mizinga mipya 300 katika vikundi vya ufugaji nyuki.

Lazaro alisema kila kikundi kimepewa mizinga 20 na sasa wameanza kuvuna asali na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu, kuwa na mavuno makubwa.

"tunapongeza TSF na Waziri wa Maliasili na Utalii, ambaye ni mbunge wetu, Dk Hamis Kigwangalla kwa kazi nzuri ambayo wanafanya hapa nzega kuwahakikisha maisha bora wananchi kupitia asali badala ya kutegemea kilimo pekee"alisema.

Posted by MROKI On Thursday, October 10, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo