Nafasi Ya Matangazo

July 01, 2019

MWANARIADHA Fabiano Joseph akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya tatu yaliyofanyika juzi wilayani hapo

MWANARIADHA Magdalena Shauri akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon yaliyofanyika juzi wilayani hapo.(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
MWANARIADHA Marco Joseph akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon yaliyofanyika juzi wilayani hapo.
MWANARIADHA Asha Samwe akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya pili yaliyofanyika juzi wilayani hapo.
MWANARIADHA Josephat Joshua akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya pili yaliyofanyika juzi wilayani hapo
MWANARIADHA Mayselina Mbua akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu mara baada ya kun'gara katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon nafasi ya tatu yaliyofanyika juzi wilayani hapo BOFYA HAPA KUONA ZAIDI

Mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu akizungumza katika mashindano hayo mara baada ya kukabidhi zawadi washindi walioongoza katika mashindano ya riadha 
Mmoja wa waandaaji wa Monduli Maasai Marathon Meja Humphrey Nyuchi ambaye ni mkurugenzi mwenza alisema lengo hasa za mbio hizo kuimarisha michezo ,elimu na afya na mbio hizo zililenga katika kutangaza vivutio na fursa zilizopo Monduli.
Kikundi cha ngoma kabila maarufu la kimaasai kikitoa burudani katika mashindano hayo,
Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akitoa zawadi shilingi elfu ishirini kwa mama aliyeshiriki mashindano hayo ya riadha huku akiwasii wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki michezo
Mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba akiwa katika picha ya pamoja na watoto walioshiriki mashindano hayo,amabapo alidhamini Zawadi za watoto zenye thamani ya shilingi laki tatu
Kikundi cha Arusha runners wakishangilia zawadi ya mbuzi (2)walizokabidhiwa mara baada ya kutajwa kuwa wahamasishaji wa zuri wa shindano hilo

Na PamelaMollel,Monduli
Mashindano ya riadha maarufu kwa jina la Monduli Maasai Maradhon imekuwa kivutio kikubwa kwa wananachi waliojitokeza kuangalia shindano hilo lililowashirikisha wadau mbalimbali 

Mashindano hayo ya riadha yaliyofanyika juzi yanatajwa kuwa mashindano ya kwanza kufanyika Monduli na kufanya washiriki mbalimbali walioshinda kujinyakulia zawadi 

Wanariadha Marco Joseph na Magdalena Shauri wamefanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya riadha ya Monduli Maasai Marathon 

Kwa wanaume waliokimbia kilomita 21 Joseph Kutoka talenti alitumia Muda wa saa 1:19:27 akifuatiwa na Josephat Joshua Kutoka Polisi kwa muda wa 1:05:54 huku nafasi ya tatu akishilia Fabiano Joseph kutoka JWTZ kwa muda wa saa 1:06:13.

Kwa wanawake Magdalena Shauri aliongoza kwa muda wa saa 1:19:27 akifuatiwa na Asha Samwe kwa muda wa saa 1:20:16 huku nafasi ya tatu ikimwendea Mayselina Mbua kwa muda wa 1:20:32.

Zaidi ya wanariadha 200 walishiriki mbio hizo za km 21,km 5 na km 2.5 ambazo ziliongozwa na mkuu wa wilaya Monduli Idd Kimanta ambapo washindi walikabidhiwa Zawadi za fedha na medali na tishirt.

Washindi kwa kilomita 21 kwa wanaume na wanawake ,Mshindi wa kwanza Alipata shilingi laki 500,000 na ,mshindi wa pili 300,000 na Mshindi wa tatu 200,000, Mshindi wa nne 150,000 na Mshindi wa Tano 100,000 pamoja na katoni za vinywaji huku Zawadi za mbuzi mnyama zilitolewa kwa baadhi ya washindi wengine.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya Monduli Meneja wa benki ya NMB Monduli Rebecca Lobulu aliwapongeza waandaaji na washiriki,huku akisistiza kuwa michezo ni fursa ya ajira na pia inaimarisha mwili

Alitoa wito kwa wazazi kuwahimiza wototo michezo na badala yake waache kubeza watoto wanaofanya vizuri katika michezo

Mmoja wa waandaaji wa Monduli Maasai Marathon Meja Humphrey Nyuchi ambaye ni mkurugenzi mwenza alisema lengo la mashindano hayo kuibua fursa zilizopo katika eneo hilo pamoja na kuimarisha michezo

Alisema ni Mara ya Kwanza mbio hizo zinazinduliwa na matarajio mbio hizo zitakuwa endelevu kwa ila maana ya kuwa zitafanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi Juni .

Naye mkurugenzi wa shule ya Upendo Friends Isabella Mwampamba ambaye walidhamini Zawadi za watoto zenye thamani ya shilingi laki tatu alisema kupitia michezo watotonwanaweza kufanya vizuri zaidi

Alisema serikali iweke mkazo zaidi kuwekeza katika michezo kuanzia ngazi za chini ili kuweza kuwa na vijana watakaofanya vizuri baadae na kuliwakilisha taifa vyema.
Posted by MROKI On Monday, July 01, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo