Nafasi Ya Matangazo

May 31, 2019

Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo Mkoani Morogoro wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea Chuoni hapo ambapo amesema ameridhishwa na kasi na ubora wa majengo yanayojengwa 


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ,Prof. Joyce Ndalichako  amekipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa usimamizi mzuri wa mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea Chuoni hapo.

Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo Mkoani Morogoro wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi unaoendelea Chuoni hapo ambapo amesema ameridhishwa na kasi na ubora wa majengo yanayojengwa 

Mradi huo unaogharimu Shilingi bilioni 6.5 unahusisha ujenzi wa Majengo manne ya ghorofa ya hosteli za wanafunzi ambayo yatachukua wanafunzi 1,024 kwa mara moja pindi yatakapokamilika. Mradi huo pia unahusisha ujenzi wa nyumba za waangalizi pamoja na maeneo ya kufulia na kuanikia nguo za wanafunzi.

Aidha,Waziri Ndalichako ametoa pongezi kwa SUMA JKT kwa kutekeleza mradi huo kwa kasi na kwa ubora huku akiwataka wakandarasi wengine wanaofanya kazi katika miradi mbalimbali ya ujenzi ya Wizara ya Elimu, Sayandi na Teknolojia kuiga mfano wa SUMA JKT katika utendaji.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kuboresha miundo mbinu ya Chuo hicho katika Kampasi ya Mbeya na Kampasi Kuu Morogoro, akieleza kuwa uwekezaji wa kiasi hicho kwa Chuo Kikuu Mzumbe haujafanyika kwa zaidi ya miaka 40. 
Posted by MROKI On Friday, May 31, 2019 1 comment

1 comment:

  1. Ni vyema mradi ukikamilika mapema. Swala la hostel limekua changamoto kwa wanafunzi wa chuo hiki kutokana na gharama za hostel za nje kua kubwa na mazingira kutokua rafiki

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo