Nafasi Ya Matangazo

February 17, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa sita toka kushoto) na viongozi wengine alioambatana nao akimsikiliza Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi (wa nne kushoto) wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni atembelea mradi wa visima unaotekelezwa unaotekelezwa na Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA) katika Wilaya yake huku akiitaka mamlaka hiyo kumaliza miradi hiyo kwa wakati. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza ziara yake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri amesema ipo haja ya kumaliza miradi kwa wakati ili kuweza kuwapa wananchi huduma stahiki. 

 "Niwashuruku DAWASA kwa kutenga baadhi ya miradi na kuisimamia mpaka ikamilike kwa asilimia 100, ili sasa tunavyotatua changamoto za wananchi tujue kwamba Kimbiji, Gezaulole na Vijibweni hakuna tatizo la maji ili tuendelee na miradi mingine kuliko kuwa na miradi mingi alafu rasilimali ni chache alafu tunaendelea kuibua miradi mingine tunakuwa na viporo ambavyo havijakamilika", Amesema Msafiri 

 Amesema Kigamboni kuna changamnoto kubwa ya miradi ya maji na umeme, kukamilika kwa wakati jambo ambalo linaweza kukwamisha ujenzi wa viwanda kwani kwa sehemu kubwa viwnada vinategemea maji na umeme wa uhakika.

 "Leo tumeanza kutembelea miradi ya maji, hasa miradi inayotekelezwa kwenye ngazi ya Taasisi ambazo hazipo chini ya Manispaa ya Kigamboni na tumetembelea miradi mbalimbali na miradi mingi ni ya muda mrefu kwa mfano mradi wa Kimbiji wenye visima 12, kwa sasa DAWASA wameona wajielekeze kwenye baadhi ya visima, wamechukua visima viwili wamalize kabisa waendelee na usambazaji wa maji kwa wananchi watu waendelee kupata maji", Amesema Msafiri.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri, akiwa ofisini kwake pamoja na maafisa wa DAWASA kabla ya kuanza ziara. Ameongeza kuwa "Lakini tuna mradi mwengine kama ule wa Geza Ulole, Maradi ule ni wa muda mrefu sana, Tafrisi yake ni nini kama taasisi, kumbe wanaweza kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya mipya yenye changamoto ya kibajeti lakini tungetumia fedha hizo kufanya marekebisho", Naye Mratibu wa Miradi kutoka DAWASA, Charles Makoye, amesema Mradi wa Gezaulole ulijengwa zamani na ndio kilikuwa chanzo kikuu cha maji kwa eneo la Gezaulole, Kibungomo na Mjimwema. "Chanzo kikuu cha mradi huu ambao umejengwa mwaka 1970 ni kisima kilichopo eneo la Gezaulole chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita 28, 000 elfu klwa saa na kilikuwa kikitumia pampu ya dizeli" Amesema Makoye. Ameongeza kuwa Mradi huo ulikarabatiwa na DAWASA baada ya kuacha kufanya kazi kwa zaidi ya 18. Amesema ukarabati wa mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la maji kwa maeneo ya Gezaulole, Mbwa Maji na Kibungumo maeneo ambayo hayana mfumo rasmi wa maji pia Dawasa inatekeleza mradi wa maji wa Vijibweni unaoendela kujengwa ambapo Gharama kuuz a ukarabati wa mradi huo ni Tsh. 683,173,200.00.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akiwaa na viongozi wengine alioambatana nao wakimuangalia Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi akionja maji yaliyo matika moja ya kisima wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akiwa na viongozi wengine alioambatana nao wakimsikiliza Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi (wa nne kulia) wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akipata maelezo toka kwa  Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Charles Makoye (wa kwanza kushoto) juu ya mradi wa maji Gezaulole ambao ulijengwa toka mwaka 1970 na sasa DAWASA wameamua kuukarabati ili kutoa huduma ya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa DAWASA Ole juu ya mradi wa maji utakaovuka bahari kwa upande wa Kigamboni kwenda Kijichi na kuwapatia wakazi wa Kigamboni Majisafi na Salama.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiongea na wanahabari kutoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali ya maendeleo, changamoto zinazoikabiri wilaya hiyo mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi mbali mbali.
Posted by MROKI On Sunday, February 17, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo