Nafasi Ya Matangazo

February 17, 2019

Mwanariadha kinda ambaye pia ni balozi maalum wa DStv Francis Damiano damasi (mwenye namba 074) akiongoza katika kundi la wavulana wenye umri wa chini ya miaka 18 wakati wa mashindano ya taifa ya mbio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yamezalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio hizo yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Wengine ni Katibu mkuu wa shirikisho la riadha tanzania Wilhelm Gidabuday(kulia) na  Makamu rais wa shirikisho la riadha Tanzania
Wanariadha wa kundi la wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 18 wakicuana vikali katika mashindano ya taifa yam bio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yamezalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johsnon Mshana (Kushoto) akizungumza wakati wa kutangazwa kwa timu ya taifa yam bio za nyika mjini Moshi. Timu hiyo imetangazwa baada ya mashindano ya taifa yam bio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo ndiyo yaliyozalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio hizo yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro 
***************
MASHINDANO ya taifa ya Mbio za Nyika yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini moshi kwa udhamini wa DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, yamefanikisha uteuzi wa timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya dunia ya mbio za nyika yatakayofanika nchini Denmark mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

Akitangaza timu hiyo mara baada ya mashindano hayo ambayo yanaelezewa kuwa na washiriki wengi ukilinganisha na miaka ya nyuma, katibu mkuu wa shirikisho la riadha Tanzania Wilhelm Godabuday amesema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na ufanisi mkubwa kwani yameshirikisha wanariadha wengi na pia kumekuwa na wanariadha wapya ambao wameonyesha uwezo mkubwa.

Timu hiyo ya taifa inajumuisha jumla ya wachezaji 28 katika Makundi manne ambapo kundi la kwanza ni wanaume wa umri wa zaidi ya miaka 18, la pili ni wanawake umri zaidi ya miaka 18, la tatu ni wavulana chini ya miaka 18 na la nne ni wasichana chini ya miaka 18

Wachezaji watakaokua katika kundi la wanaume weney umri wa zaidi ya miaka 18 ni Faraja Damas(Arusha), Joseph Panga(Arusha), Sylvester Marco (Arusha), Stephano Huche (Arusha), Deogratius Nade (Manyara), Yohane Elisante (Arusha) na Bazil Sule (Polisi)

Kwa upande wa wanawake katika kundi hilo ni Failuna abdi (Arusha), Magdalena Shauri (JKT)Anjelina Daniel (Arusha), Amina Mohamed (Arusha), Marselina Issa (Arusha) na Neema Msuad (Arusha).

Kundi la wavulana chini ya miaka 18 litakuwa na wachezaji saba ambao ni Michael Kishimba (Arusha), Daniel Sinda (Arusha) Emmanuel Joseph (Manyara) Francis Damiano (Mbulu), Saimon Francis (Arusha) na Nicodemo Joseph (Mbulu) wakati wasichana watakuwa ni Agnes Protus (Arusha), Anastazia Ndoromongo (Arusha) Aisha Luguna (Arusha) Sara Hiti (JKT) Gace Jackson (JKT) Noela Lemmy (Arusha na Catherine Philipo (Manyara).

Kambi hiyo itakuwa chini ya jopo la wataalamu nane wakiongozwa na Kocha wa riadha Meta Petro kutoka Klabu ya Riadha ya Rift Valley. wengine ni Anthony Mwingereza (JWTZ), Anrea Panga (JKT), Thomas Tlanka (Arusha) na Juma Jambau (Singida). Mwanariadha maarufu mstaafu Marcelina Gwandu ameteuliwa kua muangalizi (Matron) wa Kambi hiyo huku Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Hamad Ndee akipewa jukumu la kuratibu mafunzo hayo

Akizungumza muda mfupi baada ya Mashindano hayo, Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania (DStv) Johnson Mshana, amesema kuwa DStv imekuwa ikishiriki kwa muda mrefu sasa katika kuinua mchezo wa riadha hapa nchini na kwamba ushiriki wao katika kufanikisha mashindano hayo ni katika mkakati wake endelevu wa kuhakikisha kuwa vipaji vya wanariadha wetu vinakuzwa na hatimaye kuweza kuliletea taifa medali katika mashindano ya kimataifa.

“Tuna mkakati kabambe wa ‘Ni Zamu Yetu’ ambao lengo lake kubwa ni kuhakikisha kuwa wimbo wetu wa taifa unapigwa katika michuano ya Olympic – hii ikimaanisha kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata medali katika mashindano hayo makubwa “ alisema Mshana na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo pia kutaifanya riadha kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya ajira na kipato kwa wanariadha na taifa kwa ujumla huku pia ukiwa ni ulingo mzuri wa kuitangaza nchi yetu kimataifa.

Timu hiyo ya taifa itaweka kambi jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya dunia kambi ambayo inafadhiliwa na DStv na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Posted by MROKI On Sunday, February 17, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo