Nafasi Ya Matangazo

January 13, 2019

Meneja wa kampuni ya Mwiba,Mark Ghaui (wapili kushoto) akiwa na meneja maendeleo ya jamii na Mahusiano ya Mwiba,Alfred Mwakivike (kushoto0 wakikabidhi funguo na kadi ya gari aina ya Landcrusser  waliyotoa kwa  hifadhi ya jamii ya Wanyamapori ya Makao na viongozi wa jumuiya hiyoanayepokea ni Mwenyekiti ni Kaimu Mwenyekiti Nzemo Gwesere akiwa na Katibu wake Robert Simon .
Meneja wa kampuni ya Mwiba,Mark Ghaui (wapili kushoto)akiwa na meneja maendeleo ya jamii na Mahusiano ya Mwiba,Alfred Mwakibiki (kushoto)  baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuwekeza shughuli za Utalii,katika hifadhi ya jamii ya Wanyamapori ya Makao na viongozi wa jumuiya hiyo,Robert Simon Katibu na Kaimu Mwenyekiti Nzemo Gwesere jana
Na Mwandishi wetu,Meatu.
Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori (WMA) ya Makao,iliyopo wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu,juzi imepatiwa msaada wa gari aina ya Toyota Land Crusser baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa utalii wna uwindaji na kampuni ya Mwiba Holdings limited.

Mkataba huo, ulisainiwa katika halmashauri ya Meatu, ambapo katika kipindi cha miaka mitano,Makao WMA itakuwa ikipata fedha wastani wa shilingi 600 milion kutoka sh 400 milioni za miaka mitano iliyopita.

Akizungumza katika makabidhiano ya gari hilo, lenye thamani ya sh 40 milioni, baada ya kusaini mkataba, Meneja wa Mwiba Holdings moja ya kamapuni ya Friedkin Conservation Fund, Mark Ghaui alisema wanatarajia ndani ya miaka mitano kuongeza watalii katika eneo hilo.

"tumetoa msaada huu wa gari, ili litumike katika doria za ulinzi wa wanyamapori na mazingira na tutaendelea kutoa misaada mingine ili kuhakikisha jamii pia inanufaika na uhifadhi"alisema kwa upande wake, Katibu wa Makao WMA, Robert Simon  licha ya kushukuru msaada huo, pia alitangaza operesheni ya kuwaondoa watu waliovamia maeneo ya hifadhi.

Alisema wametoa mwezi mmoja kwa kaya zaidi ya 60 zilizovamia maeneo ya hifadhi ili kutoka na hivyo kuendelea kutunzwa kwa mazingira ya hifadhi hiyo.

Alisema mkataba waliosaini, umeboreshwa kwani fedha za kila kijiji zimeongezeka kutoka wastani wa sh 25 milion hadi 27 milioni na kwa mwaka fedha zimeongezeka hadi kufikia 600 milioni.

Kaimu Mwenyekiti wa Makao WMA, Nzemo Gwesere alipongeza kampuni ya Mwiba kwa kusaini Mtakaba mpya na Makao WMA na kutoa gari kwa ajili ya ulinzi.

Alisema Makao WMA na serikali kwa ujumla katika miaka mitano ijayo itanufaika zaidi na uwekezaji wa kampuni hiyo kwani watalii wataongezeka.

Posted by MROKI On Sunday, January 13, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo