Nafasi Ya Matangazo

January 11, 2019

Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa huo kutumia fursa ya upatikanaji wa bima ya msingi hili kujiwekea nafuu ya Maisha kama alivyoagiza Rais Magufuli.

Makonda amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mpango mpya wa bima ya afya ya msingi kwa wakazi wa mkoa huo.“Bima hii ni nafuu san asana kwani familia ya watu sita itaweza kulipa kiasi cha Shilingi laki moja na amsini tu huku mtu ambaye atakuwa anaishi peke yake atalipa shilingi elfu arobaini kwa mwaka”amesema Makonda

Amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam umeandaa wataalamu Zaidi ya 1000 ambao watakuwa wanapita kila mtaa katika wilaya zote tano hili waweze kuandikisha kila kaya kuweza kupata huduma hii.

Makonda ametaja kuwa uwepo wa Bima hiyo ya Msingi utasaidia watu kuacha kuchangishana kwa ajili ya mtu katika familia kuchangiawa kwa ajili ya matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mpango wa bima ya aAfya unaotolewa na mkoa wa Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Dr. Grace Maghembe akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mpango wa bima ya Afya unaotolewa na mkoa wa Dar es Salaam.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF na CHF),Nicholaus Mwangomo akieleza na namna mfumo wa bima ya msingi utakavyowasaidia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Mshauri kiongozi wa HPSS, Ally Kebby akizungumza namna gani walivyojipanga kukamilisha mpango wa bima ya msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Waandishi wa Habari wakifatilia Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda juu ya mpango wa bima ya aAfya unaotolewa na mkoa wa Dar es Salaam.

Posted by MROKI On Friday, January 11, 2019 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo