Nafasi Ya Matangazo

December 05, 2018

Gari alilojishindia Bw.Frank Nathan hilo.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo ( wapili kushoto) akiongea kwa sim una mshindi wakati wa droo ya pili ya promosheni ya TBL Kumenoga iliyofanyika jijini Dar Salaam. Kushoto ni Meneja masuala endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi, , Asam Keta na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Abigail Mutayoberwa
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo ( katikati) akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa droo hiyo.Kushoto ni Meneja Masuala Endelevu wa TBL ,Irene Mutiganzi na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo Abigail Mutayoberwa. 
*********************
Mkazi wa Iringa Bw, Frank Nathan (38), amejishindia gari mpya aina ya Renault KWID, kupitia droo ya pili ya promosheni ya wateja ya TBL Kumenoga, Tukutane Baa’iliyofanyika jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha. 

Nathan, akiongea baada ya kupigiwa simu na Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema kwa furaha kuwa anayo furaha kuona ndoto yake ya muda mrefu ya kumiliki gari inatimia kupitia promosheni hii. 

“Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru TBL kwa kufanikisha ndoto yangu ya kumiliki gari “alisema kwa furaha. Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL alimpongeza mshindi huyo na kutoa wito kwa wateja wote wa vinywaji vya TBL nchini, kuendelea kuichangamkia promosheni hii ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWID.  
“Tunayo furaha kubwa kumpata mshindi wa pili wa zawadi kubwa ya mwezi ambayo ni gari mpya, kwa sasa imebaki gari moja na zawadi nyinginezo nyingi kwa ajili ya wateja wetu watakaoshiriki promosheni hii hususani katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye msimu za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya” alisema Tarimo. 

 Tarimo, aliongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa wiki yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia bia za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager. Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, alisema promosheni inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5,000 nchini kote. 

“Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.’ 

 Alifafanua zaidi kuwa ili kuingia kwenye droo ya kujishindia gari jipya kupitia promosheni hii ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ mteja atatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni, ambapo atapatiwa kuponi yenye namba, kisha anatakiwa kutuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wateja wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. 

Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz.
Posted by MROKI On Wednesday, December 05, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo