Shirika
la Ndege linaloongoza Tanzania, Precision Air, leo hii limeshiriki katika
jitihada za kuhifadhi mazingira katika maeneo ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Katika
kutimiza zoezi hilo, wafanyakazi wa shirikika hilo wakishirikiana na wanakijiji
wa kijiji cha Ngarony pamoja na wafanyakazi wa wilaya ya siha wakiongozwa na Mkurugenzi
mtendaji wa Wilaya ya Siha,Onesmo Buswelu wamefanikishaa upandwaji wa miti 1000 (elfu
moja) katika eneo linalotenganisha kijiji cha Ngarony na hifadhi ya mlima
Kilimanjaro.
Akizungumzia tukio hilo Meneja Masoko na
Mawasiliano wa Precision AirHillary Mremi amesema, Precision Air inatambua
inawajibu wa kuutnza mlima Kilimanjaro kwani mlima huo una mchango wa moja kwa
moja katika shughulli za shirika hilo.
“Mlima
Kilimanjaro unatutunza vyema sisi kama shirika na kama taifa kupitia utalii,
hivyo sote tunawajibu wa kuutunza mlima huu na mazingira kwa ujumla wake.” Mremi aliongeza.
Precision
Air imekua ikifanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka ishirini na
nne (24) na kama mdau mmojawapo wa utalii, limefanya zoezi la upandaji wa miti ikiwa
ni moja ya jitihada zake za kuhakikisha jamii inayo uzunguka mlima inaendelea
kufaidika na uwepo wa mlima, amboa ni moja ya kivutio muhimu cha utalii nchini.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Siha, Siha Valerian, amesema kuwa Shirika la
Ndege la Precision Air limeonyesha mfano
wa kuigwa na wadau wengine wa mazingira na utalii.
Valerian Ameongeza kuwa ni
wakati sasa wa kuchukua hatua madhubuti kulinda mazingira yetu ili vizazi
vijavyo viweze kufaidika na uzuri wa nchi yetu wa vivutio kama mlima
Kilimanjaro na vingine.
Mlima
Kilimanjaro ndio mlima mrefu zaidi
barani Afrika, ukiwa na urefu wa takribani mita 5,895 kutoka katika usawa wa
bahari, pia ndio mlima mrefu zaidi duniani uliosimama wenyewe (Bila kutegemea
kanda za milima).
Shirika la Ndege la Precision Air
lilianzishwa mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi, likifanya
safari zake kusafirisha watalii katika vivutio vya utalii kama Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro pamoja na Visiwa vya Zanzibar.
Sasa Shirika
hilo lenye makoa yake makuu katika Jiji la Dar es Salaam limeendelea kukua na
kuwa moja ya mashirika yanayo heshimika katika ukanda wa Africa Mashariki na
Africa kwa ujumla.
Ikifanya safari zake kutokea Dar es Salaam, Precision Air
inasafiri kuelekea Arusha, Bukoba, Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza, Tabora, Kahama,
Zanzibar,Nairobi na Entebbe.
0 comments:
Post a Comment