Nafasi Ya Matangazo

April 30, 2018

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akifungua mkutano wa wadau kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Chama cha Wenye Viwanda na Kilimo, (TCCIA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kujadili masuala ya fidia kwa wafanyakazi kutoka mikoa ya Njombe na Iringa. Mkutano huo umefanyika mjini Iringa ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kilele cha Siku ya Wafanyakazi nchini ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Iringa.
 Katinbu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, akizungumza kwenye mkutano huo.
 Mhe. Waziri akifafanua jambo wakati wa hotuba yake.
 Mtendaji Mkuu wa ATE, Bw. Aggrey Mlimuka akizungumza.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
Mshiriki akiuliza maswali ili kupata ufafanuzi 
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (katikati), akiwa na Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kulia) na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, akifafanua baadhi ya hoja kutoka kwa washiriki. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
 Baadhi ya washiriki wakipitia kipeperushi chenye taarifa za Mfuko
 Mhe. Waziri akisalimiana na wafanyakazi wa WCF wakati akiwasili.
 Baadhi ya washiriki
 Baadhi ya washiriki
 Baadhi ya washiriki
 Baadhi ya washiriki

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, akizungumza mwanzoni mwa mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anselim Peter.

Mhe. Waziri akizungumza jambo na viongozi wa WCF, na wadau wengine
Wanufaika wa fidia mahala pa kazi (mstari wa mbele), wakijumuika pamoja na washiriki wa mkutano huo.
Baadhi ya washiriki
Mshiriki akijisajili
Baadhi ya washiriki
Baadhi ya washiriki
Picha ya pamoja

NAIBU WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU,(KAZI, AJIRA NA VIJANA)  ANTHONY MAVUNDE AFUNGA MKUTANO HUO
 Katika hotuba yake ya kuahirisha mkutano huo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Anthony Mavunde, (pichani juu), amewashukuru washiriki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo, ambao lengo lake kuu ni kuendelea kuelimishana kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi na kuhimiza waajiri kujisajili na Mfuko. "Napenda kusisitiza kwamba, Mfuko huu uko kwa ajili ya kuwasaidia sio tu wafanyakazi bali pia waajiri. "Nakumbuka tulilazimika kuwapeleka mahakamni baadhi ya waajiri walioshindwa kutekeleza takwa la kisheria la kujisajili na Mfuko, nia yetu haikuwa kuwazalilisha waajiri bali ni jitihada za kuwakumbusha wajibu wenu.": Alisema, na kutolea mfano wa trafiki anapomuadhibu dereva kwa kutokufunga mkanda, na tafsiri kwamba trafiki anajali sana usalama wako kuliko wewe unavyojali usalama wako na hii si sawa, alisema. Aidha naibu waziri ameutaka Mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wadau, ili waweze kutekeleza sharia bila kisingizio chochote.
 Naibu Waziri Mavunde akipongezwa na Bw. Mshomba baada ya kufunga mkutano huo. Kulia ni Mtendaji wa ATE, Bw. Aggrey Mlimuka.
Mhe. Naibu Waziri akiongozana na Bw. Mlimuka baada ya kufunga mkutano huo.
********************
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, IRINGA
TANZANIA inaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya wafanyakaz Duniani (Mei Mosi), ambapo Serikali imewakumbusha waajiri kote nchini, kuhakikisha haki za mfanyakazi zinalindwa.


Wito huo umetolewa mjini Iringa leo Aprili 30, 2018 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama kwenye mkutano wa wadau kati ya serikali, waajiri, pamoja na sekta binafsi kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi.

Mkutano huo ambao ulikuwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi inayofanyika kitaifa mkoani Iringa, umewaleta pamoja wanachama wa chama cha waajiri nchini, (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, (TPSF), Taasisi ya Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo, (TCCIA), na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF). 


Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na ndio maana inasisitiza mazingira salama na endelevu ya mfanyaklazi mahala pa kazi ili shughuli za uwekezaji ziendelee kwani nguvu kazi (wafanyakazi), watawajibika zaidi katika kufanya kazi kwa vile wanatambua kuwa haki zao zinalindwa ikiwa ni pamoja na kulipwa fidia stahiki endapo watadhurika wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi.

Jenista alisema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika viwanda, hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia majukumu ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao za uzalishaji. 


“Tumekutana hapa leo ili kuelimishana, wajibu wetu kama waajiri, tunapaswa kuhakikisha haki za mfanyakazi zinalindwa na haki hizo ni pamoja na wewe mwajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ili kumuhakikishia mfanyakazi kuwa endapo ataumia, kuugua au kufariki wakati anatekeleza wajibu wake, basi atalipwa fidia stahiki kulingana na madhara aliyoyapata na wategemezi wake watalipwa fidia endapo mfanyakazi huyo atafariki na chombo pekee chenye jukumu la kufanya hivyo ni WCF.” Alisema 


Akieleza zaidi kuhusu faida za mwajiri kujiunga na Mfuko huo, Mhe. Waziri alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema malipo ya fidia kwa mfanyakazi aliyefariki ilikuwa ni shilingi 83,000/= ambazo walilipwa wategemezi wake.


“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Waziri.


Aidha Mhe. Waziri alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.


“Pamoja na uchanga wake, Mfuko huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili kwenye mfuko wetu ni 13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga wakiwa kazini wameshalipwa fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni 2.52 kufikia Februari 2018.” Alibainisha.


Alisema Mfuko umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia majukumu haya ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao za uzalishaji. 


“Rais wetu wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati tunapokutana kwenye baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi wasaidizi wake, kama kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri kwamba jambo hili bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi mawaziri kuchukua hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na kushauriana na wadau husika ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja na ndio maana leo tuko hapa.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.


Wakitoa ushuhuda mbele ya washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga ya kuumia au kufiwa na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo kwani umekuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi.


Akitoam ushuhuda huo, mfanyakazi wa Kampuni ya Frank Pile International Project Limited ya jijini Dar es Salaam, Bw. Patrick Millinga, yeye alisema Mfuko umemlipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 31.9 baada ya kupoteza jicho lake la kushoto kutokana na kugongwa na kipande cha chuma wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.


Mwingine aliyetoa ushuhuda wa faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi. Petronila Mligo, ambaye yeye alifiwa na mumewe katika ajali ya gari wakati akirejea kituo chake cha kazi jijini Mwanza akitokea Dodoma.


“Mfuko umenilipa fidia ya mkupuo kutokana na kifo cha mume wangu, lakini pia ninaendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi mimi na watoto wangu wawili, ambapo kila mtoto analipwa shilingi 175,000/= na mimi ninalipwa shilingi 375,000/=.” Alisema mama huyo mjane ambaye ni mwalimu.

Akiwasilisha mada mbele ya washiriki, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema Mfuko unaendeshwa kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo ina uwakishi wa serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo Shirika la Kazi Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa wafanyakazi. 


Alisema, katika mfumo wa zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa na tatizo njiani sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo inaeleza mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au akielekea kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.

“Alisema Mfuko umeweka utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa haraka na rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi kifupi.” Alisema.
Posted by MROKI On Monday, April 30, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo