Nafasi Ya Matangazo

April 29, 2018

 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akimkabidhi Vifaa vya michezo Mwalim wa shule ya seminary ya Mtwara Sisters Philipo Milanzi
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akipokea zawadi ya Mpira kutoka kwa Brand Meneja wa Cocacola Tanzania Sialovise Shayo katika uzinduzi wa Mashindano ya Copa cocacola Umisseta Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya Avod Mmanda akikagua moja ya Timu zinzoshiriki katika Mashindani ya copa cocacola Umisseta mkoani Mtwara.
Na Joseph Mpangala, Mtwara.
Mashindano ya Copa CocaCola Umisseta 2018 yamezinduliwa rasmi katka mkoa wa Mtwara.

Akizindua mashindano hayo kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara, ambaye ni mkuu wa wilaya, Evod Mmanda ametaka washiriki ambao ni wanafunzi kuyatumia kuboresha afya na akili ili kuepuka kushiriki katika matendo ya kihalifu kama matumiz ya madawa ya kulevya na kutojihusisha na mapenzi kabla ya wakati.

Mmanda amesema michezo inajenga afya na kuboresha mwili na kusema mwanafunzi atakayejihusisha katika mapenzi na kumpa mwenzake ujauzito sheria zitachukuliwa kama ilivyo kwa watuhumiwa wengine hivyo watumie muda huo kushiriki michezo.

“Hakuna muda wa ziada usiotumika vizuri wa kwenda kufanya mahusiano yaliyo nje ya utaratibu yanayopelekea mapenzi kwa watoto wa shule wote wa pande mbili,sheria iko pale pale atachukuliwa hatua kama mtu mwingine kwa watoto wa kike wakiwa kama waathirika wa kwanza na watoto wa kiume,ukamataji unakamata vile vile,”amesema Mmanda

Brand meneja wa Coca Cola Tanzania, Sialovise Shayo amesema kikubwa kinachofanyika ni kugawavifaa vya michezo kwa mpira wa miguu na mpira wa kikapu na kutoa viburudisho vinavyozalishwa na kampuni hiyo kwa wanafunzi.

“Kama kampuni tunaamini vijana ili wawe imara kakili ni lazima wafanye michezo hivyo tunawapatia vifaa vya michezo,maji na Cocacola kwasababu vipaji haviboreshi tu elimu lakini pia wakiwa wachezaji bora wanaweza kucheza lgi za kimataifa kama anavyofanya Mbwana Samata,”amesema Shayo
Posted by MROKI On Sunday, April 29, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo