Nafasi Ya Matangazo

April 11, 2018

MTOTO Michael Kadungala (15) mwenye ulemavu wa kutoona  amemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Magufuli amsaidie  aweze kupata matibabu ya tumbo kujaa maji.
Kadungala ambaye mpaka sasa ameshatoa zaidi ya lita 100 za maji katika tumbo lake lakini maji bado yamejaa katika tumbo hilo.
Akizungumza kwa taabu na Waandishi wa Habari,nyumbani kwa Mjomba wake,Joshua Msemwa eneo la Ipagala Mkoani hapa,Kadugula alisema anapenda kusoma lakini anashindwa kutokana na tumbo lake kujaa maji.
Alisema alikuwa akisoma katika shule ya wasioona ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani hapa lakini alirudishwa nyumbani kutokana na tumbo kujaa  maji.
“Mheshimiwa Rais mimi sioni na wewe ni Rais wa wanyonge nataka kurudi shuleni,naumia sana ninapoona wenzangu wanaenda shule, naumia sana naomba nisaidie niweze kupata matibabu,nakuomba sana,”alisema huku akilia.
Kwa upande wake Mjomba wake,Joshua Msemwa alisema Kadugula alianza kuumwa 2014 na walimpeleka katika Hospitali ya St Gasper ya Itigi na kutoa lita 28 za maji tumboni.
Alisema mwaka 2015 walimpeleka katika hospitali ya St Gemma ya Mkoani Dodoma ambapo alipimwa na kuonekana  hasumbuliwi na ugonjwa wowote.
Msemwa alisema mwaka 2017  ilibidi wampeleke Hospitali ya  Rufaa ya Muhimbili na kupimwa kila kitu lakini hakuna kitu chochote kilichoonekana.
“Zaidi ya kupewa  dawa za TB,lakini kila siku amekuwa akitolewa maji tumboni namuonea huruma sana Mjomba    wangu kwani haoni,Hivi karibuni tulimpeleka katika Hospitali ya Benjamini Mkapa walipima kila kitu lakini hakuna kilichoonekana,”alisema
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya wasioona ya Buigiri  Wilayani Chamwino,Happines Mgombela alisema,Kadugula alishindwa kuendelea na masomo mwaka 2014 akiwa darasa la nne kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa tumbo kujaa maji.
“Sasa hivi ndio angekuwa akimaliza darasa la saba kiukweli darasani alikuwa yupo vizuri alikuwa akishika nafasi tano za juu hasa mbili au tatu,”alisema
Naye Mbunge wa Jimbo la Kilolo,ambaye pia ni Balozi wa wasioona nchini,Venance Mwamoto  alisema amejitahidi kwa kila hali kuhakikisha Kadugula anapata matibabu lakini kwa sasaamefikia mwisho.
Kutokana na hali hiyo,Mwamoto   amemwomba Rais  Rais Dk.Magufuli na wadau mbalimbali wamsaidie ili mtoto huyo aweze   kupatiwa matibabu.
Kauli hiyo pia inaungwa Mkono na Diwani wa Kata ya Buigiri Keneth Yindi (CCM). 

Yeyote Mwenye kuguswa kwaajili ya kumsaidia mtoto huyu Matibabu awasiliane na Mjomba wake 0755090234 JOSHUA MSEMWA.
Posted by MROKI On Wednesday, April 11, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo