Nafasi Ya Matangazo

April 24, 2018

 Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akipunga mkono kuonyesha ishara ya moto wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv NI MOTO’. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam ambapo pia DStv ilitangaza kuwa itarusha matangazo ya Kombe la dunia kwa lugha ya Kiswahili
 Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria (kulia) na mwenzake wa Masoko Salum Salum (Kushoto) wakionyesha ishara ya moto wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv NI MOTO’. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam ambapo pia DStv ilitangaza kuwa itarusha matangazo ya Kombe la dunia kwa lugha ya Kiswahili. Wengine (kutoka kulia) ni mabalozi wa DStv Khadija Kopa, Soudy Brown, Riyama Ally na Nancy Sumari.
 Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akipunga mkono kuonyesha ishara ya moto wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv NI MOTO’. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam ambapo pia DStv ilitangaza kuwa itarusha matangazo ya Kombe la dunia kwa lugha ya Kiswahili
KATIKA kuelekea msimu wa kombe la Dunia 2018, Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia king’amuzi chake cha DStv imezindua kampeni mpya ifahamikayo kama DStv ni moto! Mteja wa DStv sasa anaweza kujiunga na huduma iitwayo “DStv Now” na kutazama vipindi vya DStv wakati wowote mahali popote ikiwa ni pamoja na kupata fursa ya kuunganisha vifaa vitano (5) zaidi ikiwemo simu ya kiganjani, Tablet, Laptop au Desktop pamoja na Runinga. 
Hii inamaanisha watu wa tano (5) tofauti wanaweza kutazama huduma ya DStv kupitia vifaa vitano (5) tofauti kwa wakati mmoja na kwa akaunti moja tu ya malipo ya mwezi!

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaa Jana, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Alpha Mria alisema “Wakati tunaelekea kwenye mashindano makubwa kabisa ya soka Duniani yaani Kombe la Dunia la FIFA , tunampa fursa mteja kutazama huduma ya DStv kwenye vifaa hadi vitano kwa wakati mmoja. 
Hii itawaondolea wateja wetu usumbufu na sintofahamu hususani pale watu wengi wanapotaka kutazama vitu tofauti wakati wowote mahala popote kwa wakati mmoja“

Aliongezea kusema “Tumekuwa tukiboresha huduma zetu kila uchao hususan kuongeza maudhui na pia kuwarahisishia wateja wetu utazamaji wa vipindi mbalimbali tena kwa kiwango cha hali ya juu kabisa“ alisema Alpha na kuongeza kuwa App hiyo ya DStv Now inapatikana kwa wateja wa vifurushi vyote.

Alpha amesema kwa kuzingatia uzito wa michuano ya Kombe la dunia mwaka huu, DStv imejipanga kuhakikisha kuwa watanzania wanapata fursa ya kuona mechi zote zikiwa katika mfumo wa HD, na pia kwa bei nafuu sana na kwa jinsi watakavyo wateja.
 “Kwanza tunakupa fursa ya kutazama kombe la Dunia popote ulipo iwe ni kwenye laptop, tablet, simu, au kwenye runinga yako; ni chaguo lako na ndiyo sababu tunasema Burudika popote ulipo na DStv.. DStv ni moto!“

Pia amebainisha kuwa DStv itakuwa ikirusha matangazo ya michuano hiyo kwa lugha ya kiswahili kwa kuwatumia watangazaji nguli wa michezo hapa nchini. Amesema kuwa kumekuwa na maombi mengi sana kutoka kwa wateja kutaka matangazo hayo yarushwe kwa kiswahili hivyo DStv imetimiza matakwa ya wateja wake na sasa itarusha matangazo hayo kwa Kiswahili.

Kujiunga na huduma ya “DStv Now”, mteja anapaswa kupakua App ya DStv Now kupitia Simu yake ya mkononi au Tablet ama Laptop na Desktop ataingia DStv.com kisha kufuata maelekezo na kisha kujisajili kwa kuweka taarifa zake muhimu ikiwemo email (barua pepe) namba ya simu pamoja na Smartcard number ya DStv. Baada ya hapo mteja anaweza kufurahia huduma ya DStv wakati wowote mahali popote. Huduma hii inapatikana kwenye vifurushi vyetu vyote vya DStv.

Amewataka wateja wa DStv na watanzania kwa ujumla kukaa mkao wa kula kwani kuna mambo makubwa sana kutoka DStv msimu huu wa kombe la Dunia. “Huu ni mwanzo tu wa moto wa Kombe la Dunia, siku chache zijazo tutasikia makubwa zaidi kutoka DStv kuhusu mashindano haya “

Kama hiyo haitoshi, kuanzia April 18 mwaka huu, DStv iliongeza chanel maalum DStv 214 inayopatikana kwenye vifurushi vyote, ambayo ni mahususi kwa amsha-amsha za kombe la Dunia. 
Channel hii huelezea historia na matukio muhimu ya Michuano hiyo na pia kuonyesha mechi kadhaa za michuano iliyopita bila kusahau makala maalum, mahojiano na wadau na wataalamu mbalimbali wa soka na matukio yote yaliyotikisa michuano hiyo kwa miaka iliyopita.

Zaidi ya hayo, DStv inaendelea kukupa maudhui moto moto hasa kipindi hiki cha kulekea msimu wa Kombe la Dunia, kwani utashuhudia fainali za UEFA champions League, Fainali za Europa League, Fainali za FA Cup, Na mwisho wa msimu wa Premier League na Laliga bila kusahau Filamu na Tamthilia kali za kusisimua za ndani na nje ya nchi, WWE Mashindano ya Mieleka, vipindi vya mapishi, watoto na vingine vingi, Hakika ni DStv NI MOTOOO!!
Posted by MROKI On Tuesday, April 24, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo