Nafasi Ya Matangazo

March 04, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 
Klabu ya Simba inatarajia kucheza mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi ya klabu ya Al Masry kutoka nchini Misri siku ya Jumatano ya tarehe 7/3/2018 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza mishale ya saa 12 kamili jioni, Aidha viingilio katika mchezo huo vinataraji kuwa katika bei zifuatavyo;-

I. VIP A – Tsh 20000
II. VIP B - Tsh 15000
III. Mzunguko/Orange – Tsh 5000.
 
Tiketi za kuingilia uwanjani siku hiyo zitaanza kuuzwa siku ya Jumatatu kwa mawakala wa Selcom na vituo vitakavyotangazwa hapo baadae.

Klabu inawaomba mashabiki na wapenzi wa klabu kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuishangilia timu yao itakapokuwa inacheza, aidha inawakumbusha kununua tiketi za mechi hiyo kwa wakati.

Katika hatua nyingine,Klabu ya Al Masri inataraji kuwasili nchini siku ya Kesho Jumapili majira ya saa 12 jioni,na itafanya mazoezi siku ya Jumatatu jioni katika Uwanja Taifa.

Pia,waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Afrika kusini wanatarji kuwasili nchini siku ya Jumatatu saa 10 jioni.

Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,

Simba Sports Club,
Haji S. Manara
3/3/2018 

Simba Nguvu Moja..!!!
Posted by MROKI On Sunday, March 04, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo