Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2018

Mashine za kushonea nguo zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum (Vijana) Mkoa wa Kigoma, Zainab Katimba vikikabidhiwa kwa vikundi vya vijana.
Mbunge wa Viti Maalum (Vijana) Mkoani Kigoma, Zainabu Katimba (kulia) akiwa katika makabidhiano hayo ya mashine za kushonea nguo.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
UMOJA wa Vijana wa chama cha mapindizi UVCCM mkoa wa Kigoma Wametakiwa kuachana na siasa za Maneno na kufanya siasa za uchumi ilikuweza kuunga mkono kauli mbio ya Rais John Magufuli ya kuanzisha Viwanda.

Wito huo ulitolewa jana na mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa MNEC, Kilumbe Ngenda ambae alikuwa Mgeni rasmi, Katika Baraza la Vijana wa UVCCM Mkoa wa Kigoma katika uchaguzi wa wajumbe watatu wa kamati ya utekelezaji ya uvccm mkoa na kumthibitisha katibu wa uhamasishaji na chipukizi,ambapo aliwataka Vijana hao kubuni miradi na kuendeleza miradi waliyonayo kama jumuiya nyingine zinavyo fanya.

Alisema Vijana wanatakiwa kuwa na miradi yao binafsi ilikupunguza tabia ya kutembea na mabakuli kuomba, na kuahidi kutoa mifuko 50 ya Simenti ilikuweza kubuni mradi ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda pamoja na kuiboresha nyumba ya wageni ya Vijana iliyopo Manispaa ya Kigoma ujiji ilikuinua uchumi wa Vijana.

Aidha Mbunge wa Viti Maalum (Vijana) Mkoani Kigoma, Zainabu Katimba, alisema Yeye kama Kiongozi wa vijana ameamua kutoa kiasi cha shilingi milioni saba kwaajili ya kuwasaidia vijana Wilaya zote kuanzisha miradi pamoja na kuanzisha viwanda na kutoa Vyeleani vitatu Katika Kikundi cha Vijana wajasiliamali wa Kikundi cha Mwandiga.

Alisema wanaendelea na jitihada za kuhakikisha Vijana wote wanakuwa na shughuli za kufanya na kila Wilaya watatakiwa kubuni miradi na wao kama viongozi watahakikisha wanasaidia kuwawezesha ilikuanzisha vikundi vya ujasiliamali pamoja na kuanzisha viwanda ilikuwajengea ajira vijana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Wa Kigoma, Silvia Sigura alisema Wao kama vijana Wamejipanga kufanya siasa za uchumi na sio siasa za maneno na kwakudhihilisha hilo wameanza kwa kukuanzisha harambee kwaVijana katika baraza lililofanyika na kufanikiwa kuchangisha mifuko 130 kwaajili ya kuanza kujenga vibanda 12 katika kiwanja chao.

Alisema kwa michango walioipata watahakikisha wanaanzisha miradi kwa kila Wilaya na kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana iliwaweze kujiajili katika masuala ya ujasiliamali na kuwawezesha vijana kuanzisha viwanda na kujiinua kiuchumi.
Posted by MROKI On Wednesday, March 07, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo