Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2018

Meneja ufundi kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka Kigoma (KUWASA) ambaye pia ni Kaimu mkurugenzi Mhandisi Mbike Jonas(kushoto) akitoa maelezo ya mradi wa maji wa Bangwe kwa viongozi wa CCM Mkoa wa Kigoma waliotembelea mradi huo.
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
UJENZI wa mradi wa maji wa Bangwe katika manispaa ya kigoma ujiji mkoani kigoma ume endelea kusuasua licha ya serikali kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo.

Mradi huo ambao kwa mkataba wa awali ulioanza mwaka 2013 ukitekelezwa na kampuni ya ukandarasi ya spencon kutoka Nchini Kenya  ulikuwa ukamilike mwaka 2015 lakini bado umeendelea kusuasua kwa kile kinachotajwa kuwa mkandarasi hana uwezo mdogo wa kifedha.

Mnamo 21 Julai, 2017 Rais Dk John Magufuli aliweka jiwe la msingi katika mradi huo na kumtaka mkandarasi huyo wa kampuni ya Spencon ya nchini Kenya kukamilisha kazi hiyo ifikapo Novemba thelathini agizo ambalo bado halijatekelezwa.

Ni mradi ambao ndio tegemeo kubwa la utatuzi wa changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa maji kwa wakazi wa manispaa ya kigoma ujiji ukitajwa kuwa pindi utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kutoa maji mara tatu ya mahitaji ya manispaa hiyo.

Mara kadhaa viongozi mbalimbali wamekuwa mstali wa mbele kufuatilia kazi hiyo wakiwemo mawaziri kwa maana ya waziri aliemaliza muda wake mhandisi Gerson Lwenge na waziri wa sasa wa maji Mhandisi Izack Kamwelwe .
Akizungumza katika ziara ya viongozi wa ccm mkoa wa kigoma ,Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Kigoma Zakaria Nicolaus mara baada ya kutembelea katika chanzo hicho alisema kuwa wao kama chama wameridhishwa na hatua ya ujenzi wa mradi ilipofikia kwani juhudi zinaonekana.

"Mmefanya kazi kubwa ya kuleta ukombozi wa maji kwa wananchi wa manispaa ya Kigoma Ujiji,sisi kama chama tumeamua kuja kuona na kujiridhisha ili tupate cha kuwaambia wananchi na cha kumwambia pia Mwenyekiti wetu wa chama Taifa"alisema

Nicolaus alisema pia mkandarasi amefanya kazi nzuri amewataka kuendelea kufanya kazi kwani wanatekeleza ilani ya chama wasipo fanya wao ndo wataadhibiwa na wananchi kipindi cha uchaguzi kinapofika.

Meneja ufundi kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka Kigoma(KUWASA)ambaye pia ni Kaimu mkurugenzi Mhandisi Mbike Jonas alisema mpaka sasa kwa eneo la katonga wateja waliounganishwa na mtandao wa maji wameanza kupata maji kupitia mradi huo mkubwa.

Alisema pia magati nane ya mradi huo yote yanatoa maji na kuna baadhi ya maeneo ya mjini pia yanapata ya mradi huo mkubwa,alisema matumaini hadi sasa ya maji kutoka mji mzima yapo kwani hadi kufika mwezi watatu mwishoni mwaka huu maji ya uhakika yatapatikana katika maeneo mengi.

"Mji wetu huu una uhitaji wa lita milioni 21 lakini mradi huu ukikamilika utatoa maji mara mbili ya uhitaji huo hivo tutakuwa na ziada ya maji ambayo tunaweza kupeleka hata maeneo mengine ambayo tupo nayo jirani"alisema

Mhandisi mshauri wa mradi huo Michael Mwamkinga alisema mpaka sasa ujenzi wa mradi huo umefikia kiwango cha asilimia 82 cha ujenzi wake,na hadi kukamilika zaidi ya Euro milioni 16 ambazo zi sawa na bilioni 32 za kitanzania zitatumika.

Baadhi ya Wananchi Mkoani kigoma wameendelea kulalamika kufuatia ahadi ya mkandarasi huyo aliyoitoa mwaka jana wakati wa ziara ya Rais kuwa mradi huo utakamilika novemba 30 mwaka jana na mji mzima …
Posted by MROKI On Wednesday, March 07, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo